Anasema wakina mama si kuwa kisa una pesa ndiyo ununue kila kitu, wengine viatu virefu hawawezi kutembelea, lakini kwasababu ana pesa amenunua kiatu kirefu.
Anasema wanaume wa Tanzania wakishaoa wanakua vilema, apelekewe maji bafuni, aletewe chakula mezani, aoshewe vyombo, hata mtoto akijisaidia anamuita mama jikoni yeye ameshika remote control.