Hapa namzungumzia zaidi Professor Palamagamba Kabudi. Huyu nguli wa sheria amekuwa ni mtu wa kuteuliwa na kutenguliwa au kuhamishwa na kurudishwa alikotoka na kuhamishwa tena kwenda kwingineko.
Professor aliteuliwa kuwa waziri wa sheria kabla ya kuhamishwa na kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje ya nchi. Baadaye Professor Kabudi aliachwa na kuondolewa kwenye baraza la mawaziri kabla ya kuja kurudishwa hvi majuzi tu kuwa waziri wa sheria na katiba.
Sasa ameondolewa wizara ya sheria ambayo ndio fani yake kitaaluma na amepelekwa wizara ya habari na utamaduni.
Tulifikiri amerudishwa mahali pake kumbe sio hivyo, nani anajua prof atahamishiwa wizara gani mwakani?
Soma Pia: Rais Samia afanya uteuzi: Masauni apigwa chini Wizara ya Mambo ya ndani, Kabudi apelekwa Wizara ya Habari na Michezo, Janabi kuwa mshauri wa Rais
Kwa maoni yangu teuzi za namna hii zinasema mengi ikiwa na pamoja na wafanya teuzi kutojua kwanini wanamteua mtu flani, kukosa mipango mkakati, kukurupuka au hata kutothamini heshima ya mtu.
Kama mtu anafaa, anafaa, kama hafai, hafai.
Nawashauri wateuliwa wa nchi hii sio lazima ukubali uteuzi kila wakati, unaweza pia kukataa.