Nafikiria kuanzisha biashara ya kuuza barafu (ice cream) naomba wazoefu mnipe ushauri

Magere Cheops

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2022
Posts
213
Reaction score
306
Habari wanna jamii.... Kama mada inavyojieleza hapo juu, ninafikilia kuanziasha biashara ya kuuza barafu katika masoko na shule zinazonizunguka ninaomba ushauri kwa wazoefu katika mambo haya
01. Kuna mashine nliwahi kuiona mahali siijui jina lakini ni Kama tank furani lina maji halafu kwa chini ndio Kuna injini unamimina juice ya barafu kwenye vyombo furani halafu unakalisha ndani ya hilo tank kwenye yale maji kwa muda mfupi tu barafu inakuwa imeganda unaitoa unaweka tena
Sasa hii mashine inaitwaje?
Inapatikana maeneo gani kwa wingi?
Bei yake ikoje
Na je matumizi yake ya umeme yakoje?
02. Hapa nilipo hakuna umeme nawaza kutumia generator kuendeshea friza
Je ni friza aina gani inaweza kuendeshwa na generator ya wastani?
Ni kwa muda gani nitawasha generator mpaka barafu kuganda?
03. Namna gani nzuri ya kutengeneza barafu zenye ladha Nzuri na zitakazopendwa kwenye soko langu hili.
Naomba kuelekezwa hapo kwa wenye uelewa wa mambo haya.
 
kama hakuna umeme usitegemee kufanya biashara ya Ice cream unakula hasara... tafuta biashara nyengine
 
Habari wanna jamii.... Kama mada inavyojieleza hapo juu, ninafikilia kuanziasha biashara ya kuuza barafu katika masoko na shule zinazonizunguka ninaomba ushauri kwa wazoefu katika mambo haya
01. Kuna mashine nliwahi kuiona mahali siijui jina lakini ni Kama tank furani lina maji halafu kwa chini ndio Kuna injini unamimina juice ya barafu kwenye vyombo furani halafu unakalisha ndani ya hilo tank kwenye yale maji kwa muda mfupi tu barafu inakuwa imeganda unaitoa unaweka tena
Sasa hii mashine inaitwaje?
Inapatikana maeneo gani kwa wingi?
Bei yake ikoje
Na je matumizi yake ya umeme yakoje?
02. Hapa nilipo hakuna umeme nawaza kutumia generator kuendeshea friza
Je ni friza aina gani inaweza kuendeshwa na generator ya wastani?
Ni kwa muda gani nitawasha generator mpaka barafu kuganda?
03. Namna gani nzuri ya kutengeneza barafu zenye ladha Nzuri na zitakazopendwa kwenye soko langu hili.
Naomba kuelekezwa hapo kwa wenye uelewa wa mambo haya.
Maelezo yako yana changanya unataka kufanya biashara ya ice cream au barafu?

Barafu ni kwa ajili ya kuhifadhia vyakula, vinywaji sehemu zisizo na umeme

Ice cream zinakuwa tamu wanapenda hasa watoto

Alafu kuna lambalamba
 
Ukisema ice cream kwa huku kwetu uswahilini huwezi kueleweka ila ukisema barafu hata katoto ambako hakajaongea kanaijua.. any way namaanisha ice cream ambazo huliwa na watoto na kina mama hapa nadhan nimeeleweka
 
Hilo tank ni mashine mkuu ndani ya hilo tank kunakuwa kuna maji chumvi na evaporator coil zinazoleta ubaridi kwanini wanaweka chumbi kwenye hayo maji wanaweka chumvi kushusha joto la maji huwa linashuka mpaka-7Centrigrade joto la maji linapokua limeshuka namna hiyo ukiweka vile vikopo(mould) ndani ya hayo maji halafu na motorninazungusha hayo maji vinaganda ndani ya muda mfupi
 
Back
Top Bottom