Nafikiria kuihama Tanzania kwenda mbali zaidi kutafuta Maisha mazuri kupitia fani yangu ya ufundi tiles

Daah, sq m TSH 2,000 mpaka nimechoka. Nipo na fundi kazi ya sqm 250 @600 per sqm 1 japo kazi zake murua
 
Tz bado kuna shida sana, tena nje ya Miji hii ndio shida zaidi.
Kwanini usitafute hizo kazi mwenyewe za kujenga tiles kuliko kusubiri kua kibarua wa fundi? Ukubaliane bei na mwenye nyumba hapo utapata ujira mzuri.
Mfano utumie kazi zako za nyuma ulizofanya kama reference uende kutafuta kazi mwenyewe.
 
Komaa bongo soko lipo. Tuliza akili Kama ulivyo aminiwa na mafundi na maboss nao watakuamini. Inshallah utapata Bei nzuri kila la kheri mpambanaji. MCHEZA KWAO HUTUNZWA.
 
Tupia kazi zako tuone umahiri wako kama kwenye wewe unabandika tiles au unajenga tiles
 
Kwa mfano UK kama umesajili kampuni yako na una vifaa vyako na vyeti vya hapa mshahara ni £71,000 kwa mwaka au kama ni mfanyakazi tu unaanza na 23,000 hadi 37,000 kutokana na experience yako
Ushauri wako mzuri apambane tu
 
Umefikia wapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…