Nafikiria kwa sauti....

mshamba_mwingine

JF-Expert Member
Joined
Jul 23, 2023
Posts
1,057
Reaction score
4,145
Leo nimekutana na hii makala mtandaoni, imenishtua na kunishangaza sana.

Mwanaume mmoja huko india ameamua kuacha kazi yake katika taasisi kubwa sana ya goldman sachs yenye mshahara mzuri, na kuwa baba wa nyumbani, ili ampe mke wake urahisi wa kupanda cheo kazini.


Anadai kwamba wanawake wengi wanakosa vyeo vikubwa kwasababu ya kujikita kwenye malezi ya watoto, hivyo wanaume wanatakiwa wajitolee zaidi kubaki nyumbani.


Vile vile anagawana na mke wake majukumu ya malezi, pale mke anapokuwa nyumbani....


Na pia ameamua(na kuridhika) kuishi kupitia mshahara wa mkewe, pamoja na akiba yao ya pamoja.


Nawaza, kama kuna wanaume wanaothubutu kufanya jambo kama hili, na likashamiri, mustakhabali wa wanaume kwenye mahusiano utakuwaje?

Wanaume tutafafanuliwa katika misingi ipi?

Hii ni sawa kweli?

Nimechanganyikiwa.
 
wahindi wana maajabu mengi kuna wengine wanagawa mali zao zote wawe maskini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…