Nafikiria usaliti waliofanyiwa 'Hawa Ghasia na Kessy', hawa watu wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru

Nafikiria usaliti waliofanyiwa 'Hawa Ghasia na Kessy', hawa watu wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,236
Reaction score
15,677
Hakuna kitu kinauma duniani kama kugeuzwa mbuzi wa kafara.

Walichofanyiwa Kessy na Ghasia huenda kikawa kichomi kimoja kibaya sana kwenye maisha yao yaliobaki hapa duniani.

"Kwanini mimi? Kwanini mimi? Yaani ina maana sina thamani kiasi hicho mpaka wanitose mimi baharini? Yaani kati ya viti zaidi ya mia mbili, wameona mimi ndo sina maana?"

Amini nakuambieni, hakuna jambo linaloumiza mwanadamu hapa duaniani kama kuanza kujiuliza "Kwanini mimi, na sio wengine?" Kutolewa kafara ni pigo kubwa sana la kuumiza nafsi.

Nashauri Hawa Ghasia na Kessy, wawekwe chini ya uangalizi maalum wasije kujidhuru.

Pamoja na kwamba watanzania wengi tumeumizwa na huu uchaguzi, ila navofikiri kuvaa viatu vya wabunge hawa wawili na wengine wachache wa CCM wataotolewa kafara, nabaki kujifariji kwamba 'matatizo ya binadamu ni mzunguko, yasipokutokea leo yatakutokea tu siki moja kwa namna tofauti'
 
Nikikumbuka yale matusi Kessy aliyo mtolea mama yule kweli Mungu ni fundi malipo hapahapa duniani

Walijua before wewe!

Huoni mada zimehamishiwa kwao wewe? Hakuna anayejadili juu ya akina Zitto, Mbowe n.k kuangushwa kwa magumashi bali mjadala umekuwa ni juu ya Kessy!

Subiri uone Kessy atapewa kitengo gani na huyo Hawa Ghasia!
Mfano huyo Mama watu hawamjui vizuri, ni threat moja kali sana kwenye kitengo!!
 
HAWA AMEWATOA SADAKA ...BAADA YA AIBU YA WABUNGE 100% LAKINI HAISAIDII....TAARIFA ZA UHAKIKA NI KUWA KWENYE VITUO VINGI VILIVYOHESABU KURA KIHALALI KABLA YA AMRI YA KUJAZA KURA BANDIA HATA BILA KUHESABU ....jpm alikuwa ameachwa mbali sana ....sana , kuna baadhi ya sehemu chache walihesabu kura angalieni nao mtaona range ya matokeo ambayo ilikuwa ni predictive ya matokeo halisi baada ya huo muelekeo na kuonekana maeneo mengi kura bandia zilishindwa kuchomekwa kwakua zilikamatwa ., waliopewa kushindwa kazi na ikiwemo sehemu nyingine baadhi ya askari na wasimamizi wengine kuvujisha siri kwa wananchi IKATOKA amri kuwa hakuna tena kuhesabu bali ...maafisa walioandaliwa walipewa maelekezo ya kujaza matokeo ya kupika katika hali ya panic ...hii imesababisha maeneo mengi kura kuwa nyingi mara dufu ya watu waliojiandikisha kwenye eneo husika .......na asilimia kuzidi ..
HII IMEKUWA AIBU AMBAYO HATA WANA CCM ASILI INAWAUMA NA WANAONA AIBU KWA HAYA MATOKEO
 
Tena Kessy alikuwa kiherehere sana, anaweza kufa kwa pressure

Karma is Bitch aisee...

Usijidanganye boss, hiyo ni mission ambayo imepangwa vyema na tiaises!
...kama huelewi huu mchezo ndio utashangilia Kessy kushindwa, lakini in fact hakuna alichoshishindwa! Zaidi kwa waliofanya hivyo ni ushindi mkubwa sana kwao na wamefanikiwa kwa kiasi chake!
 
Unapogombea ubunge kuna kupata na kukosa. Wote hao ni wazoefu na naamini wanalijua hilo. Maisha lazima yaendelee
Waliokosa sio Ghasia na Kessy peke yao, wapo wengi
 
WATANZANIA TUJIANDAE KWA MAISHA MAGUMU KUPITA KIASI ...TUNAENDA KUONDOLEWA RASMI KWENYE DUNIA YA KISTAARABU AMBAYO TULIKUWA NA NDOTO YA KUIFIKIWA NA KUWEKWA KUNDI MOJA NA NCHI ZA HOVYO DUNIANI ...ZISIZOKUWA NA USTAARABU ...

MFANO HUWEZI KUSEMA KISIWA KAMA PEMBA UNASHINDA NA SIO STRONG HOLD ...DYNAMIC YA SIASA IKO HIVYO HAKUNA CHAMA DUNIANI KINAWEZA KUKUBALIKA SEHEMU ZOTE KWENYE NCHI ....BALI DEMOKRASIA HUWA INATAKA MAJORITY ...ALICHOKUWA ANALAZIMISHA JPM NI KUTAKA KUSHINDA KWA NGUVU HADI KWENYE MAENEO AMBAYO CCM HAINA USHAWISHI ..NA KUSAHAU UKWELI KUWA HIYO NDIO SIASA HUWEZI KUPENDWA KILA MAHALI HATA UWE MALAIKA
 
Back
Top Bottom