Nojo Wemah
Member
- Aug 9, 2017
- 21
- 19
Anaitwa Maui, nilimchukua akiwa mdogo kabisaa. Kwa kipindi cha ukuaji hapo nyuma kulikuwa na watoto wa jirani walikuwa wakicheza nae na mda mwingine walikuwa wakicheza nae vibaya kwa kumpiga hali hiyo imemfanya Maui kuwa mkorofi hasa akiwa na njaa. Kuna wakati mwingine bila sababu tu anaweza akakuparua (hii hutokea mara chache chache). Nashindwa nini nifanye ili aache hii tabia ya kuparua.
Maui anatabia ingine ya kubagua msosi ambayo ni tofauti Kwa paka wengine ambao nimekuwa nikiona wanakula vyakula vya kawaida kabisa vinavyoliwa na watu wanao wafuga, sijui ni kwa nini yeye anabagua msosi, miezi miwili nyuma nilimpatia dawa ya minyoo nikidhani labda huenda alikuwa na minyoo iliyomfanya asile chakula ambacho sie tunakula lakini pamoja na kumpatia dawa ya minyoo bado Maui aliendelea na mtindo wake wa kubagua msosi. Ili ale yeye muekee samaki au nyama tofauti na hapo ali kabisa atunusanusa hapo kisha ataacha. NIFANYE NINI ILI MAUI AWE ANAKULA MSOSI BILA KUBAGUA, MBONA WENGINE HAWABAGUI?? NIJUZENIIII....