Nafuta mke aliyezaliwa 08/02/1980

Nafuta mke aliyezaliwa 08/02/1980

masanzu

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
605
Reaction score
217
Hbr wanajamvi
kama kunamdada aliye zaliwa 08/02/1980 mpaka sasa hajapata mme basi anipm na shaka aondoe amempata ila baadaye ntahitaji uthibitisho asante siku njema
 
Hivi vituko vya siku hizi kila kukicha vinaongezeka.
Haya nayo sijui ni majanga au.................
 
Hivi tafsiri sahihi ni "kutafuta mke" au "kutafuta mwanamke atayekuwa mke"?
 
Inatisha kidogo mana angalau ungesema unataka ivyo kwa sababu gani mana ni ajabu na kweli unaweza ukadhaniwa ni mwanga ama ni mchawi au una lako jambo...........ebu fafanua,yako mpya,fafanua ili usomeke!
 
kama kunamdada aliye zaliwa 08/02/1980"
Aliyezaliwa mwaka huo sio mdada ila ni mmama
 
wapi wanatengeneza birth certificate feki jamani?
 
Hbr wanajamvi
kama kunamdada aliye zaliwa 08/02/1980 mpaka sasa hajapata mme basi anipm na shaka aondoe amempata ila baadaye ntahitaji uthibitisho asante siku njema
Mkuu masanzu wewe unatafuta Mdada

aliyezaliwa 08/02/1980 wakati wewe hujatuambia umezaliwa tarehe gani? Kwanza

unajuwa huyo M-Dada aliye zaliwa Tarehe ( 08/02/1980) unajuwa Tabia yake?

NYOTA YA NDOO (AQUARIUS)

  • Hii ni nyota ya kumi na moja katika mlolongo wa nyota 12.
  • Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 20 January na 18 February.
  • Sayari yao ni SATURN (ZOHAL).
  • Siku yao ya bahati ni Jumamosi.
  • Namba yao ya bahati ni 8.
  • Rangi yake ya bahati ni Nyeusi.
  • Asili ya nyota hii ni Hewa.

KIPAJI CHA NDOO


(Sudden Revelation)

Wenye nyota hii wana kipaji cha kutoa tafsiri sahihi ya jambo lolote linalotokea wakati wowote.

TABIA ZA NDOO


Wenye nyota ya Ndoo ni watu wachangamfu, wavumbuzi na wenye akili za kubuni jambo au kitu. Ni watu ambao wenye furaha wakati wote lakini inakuwa vigumu wakati mwingine kuwa karibu nao. Ni waaminifu na wakweli na wako tayari wakati wowote kutoa msaada unaohitajika.


Kwa upande mwingine ni watu ambao hawatabiriki hasa wanapokasirika, wanaweza kuwa wakaidi, wenye kushikilia jambo hata likiwa baya, ni wapotovu wa nidhamu na waasi.


Ni watu ambao hawajali Dunia inasema nini au inafikiria nini, wakati mwingine hukataa shughuli za kijamii na kujihusisha katika mambo yasiyo na maana yeyote.


Kwa ujumla ni watu wenye Roho nzuri ya kibinaadamu wanapenda kutoa msaada pamoja na kwamba wakati mwingine wanakuwa siyo dhahiri.



TABIA YA NDOO KATIKA MAPENZI.

Wenye nyota ya Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na

miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada

mkubwa kwa wapenzi wao.


Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Ni watu
ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.


Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.


Ni watu ambao wenye kusema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.


Katika ngono kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.


Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.

UHUSIANO WA KIMAPENZI

(NDOO NA SIMBA)

Tabia ya kupenda kuwa huru na kujifanyia mambo bila kuingiliwa waliyokuwa nayo wenye nyota ya Ndoo,

huwafariji wenye nyota

ya Simba ambao nao hawapendi kuingiliwa katika mambo yao.

Haya niambie Mkuu
masanzu Mwenye kuzaliwa hiyo Tarehe( 08/02/1980) Je utamuweza kuishi nae kweli?

 
Back
Top Bottom