BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Ahueni za bei ya mafuta imezidi kuonekana kwa miezi mitatu mfululizo huku hali hii ikiakisi kushuka kwa bei za soko la mafuta la dunia.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) leo Jumanne Novemba 1, 2022 imeonyesha kuwa kuanzia kesho Jumatano mkoani Dar es Salaam bei ya petroli itabaki kama ilivyo Sh2, 886 kwa lita moja na dizeli imeshuka kidogo kwa Sh31 kutoka Sh3, 083 hadi Sh3, 082, huku bei ya mafuta ya taa ikipungua kwa Sh224 na kufikia Sh3,111.
Hata hivyo, taarifa ya wa mtandao wa ‘Trending Economics’ inaonyesha hadi Novemba 2022, bei ya mafuta ghafi kwa pipa ilikuwa ikiuzwa kwa Dola 88.56 za Marekani sawa na Sh203,688 ikiwa imeongezeka kwa Sh1,518 ikilinganishwa na bei ya Oktoba.
Bei ya mafuta ghafi imekuwa ikipungua kutoka Dola 103.6 (wastani wa Sh238,280) , kwa Julai hadi kufikia Dola 94.9 (wastani wa Sh218,270), Dola 90.4 ( wastani wa Sh207,920) Septemba na 87.9 Oktoba (wastani wa Sh202,170).
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Serikali imeendelea kutoa ruzuku kwenye bidhaa hizo ikilenga kupunguza ukali wa bei.
Serikali ilitoa ruzuku ya Sh59.58 bilioni kwa ajili ya bei za mafuta ya Oktoba 2022, ikiwa ni kiwango kidogo zaidi ukilinganisha na Sh65 bilioni iliyotolewa mwezi Septemba huku mwezi huu haijataja kiasi cha ruzuku iliyotolewa.
Kwa mujibu wa taarifa ya Ewura, Mkoa wa Tanga bei ya mafuta ya petroli imeshuka kutoka Sh2, 924 Oktoba hadi Sh2, 806 mwezi huu huku dizeli ikipungua kwa Sh34 na kuwa Sh3, 074, Mtwara bei ya petroli imepanda kutoka Sh2, 908 Oktoba hadi Sh2, 917 mwezi huu.
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU BEI KIKOMO ZA BIDHAA ZA MAFUTA YA PETROLI KUANZIA JUMATANO, TAREHE 2 NOVEMBA 2022
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zitaanza kutumika kuanzia Jumatano, Tarehe 2 Novemba 2022 saa 6:01 usiku.
Bei ya mafuta ya rejareja ya dizeli kwa Dar es Salaam na Tanga kwa Novemba 2022 imepungua kwa shilingi 31/lita na 34/lita, sawia ikilinganishwa na bei hizo kwa Oktoba 2022 kwa sababu ya ruzuku. Bei ya rejareja ya mafuta ya petroli kwa Bandari ya Dar es Salaam ingeongezeka kwa shilingi 110/lita, hatahivyo, Serikali imetoa ruzuku ili bei iliyopo ya Oktoba 2022 isibadilike. Kwa upande wa Mtwara, hakuna meli ambayo imehusishwa kwenye bei kwa Novemba 2022 kwa sababu meli inategemewa kushusha mafuta mwishoni mwa Novemba 2022 na mafuta yake yatatumika Desemba 2022. Hivyo, mabadiliko ya bei kwa Novemba 2022 kwa Mtwara ni kwa ajili ya kuhusisha taarifa sahihi ya meli husika iliyotumika kwenye bei za Oktoba 2022.
Bei ya mafuta ya taa na bei ya petroli kwa Tanga imepungua kwa shilingi 164/lita na shilingi 118/lita ukilinganisha na bei zilizopita kwa sababu ya wastani wa bei ndogo zaidi ya mafuta yaliyosafishwa katika soko la dunia na gharama za usafirisha kwa bandari ya Tanga. Jedwali Na. 1 linaonesha bei za Novemba 2022 zisizo na zenye ruzuku.
Jedwali Na. 1: Bei za rejareja zisizo na zenye ruzuku kwa Novemba 2022 (Shilingi/Lita)
Kutokana na mgawanyo wa ruzuku kwa mafuta ya petroli na dizeli, Jedwali Na. 2 linaonesha ulinganisho kati ya bei zenye ruzuku za Oktoba 2022 na bei zenye ruzuku za Novemba 2022.
Jedwali Na. 2; Bei kikomo za rejareja za Novemba 2022 ukilinganisha na Bei kikomo za rejareja za Oktoba 2022
Hivyo, bei kikomo za mafuta kuanzia tarehe 2 Novemba 2022 ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 3. Kutokana na bei hizi, bei za miji, wilaya na mikoani ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 4. Totauti ya bei kutoka sehemu moja kwenda nyingine inatokana na tofauti ya bandari mafuta yanapochukuliwa na gharama ya usafirishaji.
Jedwali Na. 3: Bei kikomo za mafuta kwa kila bandari zitakazoanza kutumika kuanzia tarehe 2 Novemba 2022 (Shilingi/Lita)
Katika kutekeleza bei hizi, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kwa ujumla wanatakiwa kuzingatia yafuatayo: -
(a) EWURA inapenda kuukumbusha umma kwamba bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana pia kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo. Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
(b) Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko.
3
EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta. Taarifa hizi zina lengo la kuwasaidia wadau kufanya maamuzi stahiki kuhusu manunuzi ya bidhaa za mafuta.
(c) Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani mradi tu bei hizo zisivuke bei kikomo (Price cap) au kushuka chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama ilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa kupitia Magazeti ya Serikali Na. 2A na 57 ya tarehe 3 Januari 2022 na 28 Januari 2022, sawia.
(d) Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana na yakionesha bei ya mafuta, punguzo, vivutio vya biashara au promosheni zinazotolewa na kituo husika. Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani. Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja. Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
(e) Wauzaji wa mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa risiti za mauzo kutoka kwenye mashine za EFPP (Electronic Fiscal Pump Printers) na Wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Stakabadhi hizo za malipo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya aidha kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora kinachofaa, na pia, risiti hizo zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya mafuta ya petroli.
(f) Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 4. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.
(g) Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei yenye ruzuku kama inavyooneshwa kwenye Jedwali Na. 5. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.