Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Waziri amekengeuka. Wametumia kigezo gani kuifanya singeli ndiyo alama ya Taifa?
Muziki wenyewe umejaa matusi nafuu ingekuwa taarab kwa kuwa yenyewe ina mfumbo. Singeli huwezi kusikiliza na watu unaowaheshimu kama wazazi au watoto, abadan.
Pili ukikuta muziki wenyewe unavyochezwa, ni mtindo wa kukosa maadili tu. Wanawake wanavaa madera mostly bila chupi, halafu wanakamata ardhi then makalio yanakuwa juu ndiyo wanaanza kuyatikisa
Kuna wimbo wa Dulla Makabila una mstari ufuatao "nakupenda wewe na huyo bwanako" ndio uwapelekee duniani utawaeleza maana yake nini? Ujinga mtupu.
Wadau wa muziki mshaurini Waziri Kabudi asitishe UCHAFU huu