tujuemoja
Member
- Jul 26, 2022
- 7
- 2
"Ni kweli mnanipinga, lakini naomba ujue na kutambua sababu ya kwa nini unanipinga"
Fanya mazoezi, kuwa na kiasi, kunywa maji safi na salama, Vuta hewa safi, ota mwanga wa jua, ndio jina langu yaani Afya bora.
Majukwaani na panda kuzinadi zangu sera lakini wanaoshawishika ni wachache, kwa hoja dhaifu za kupinga mazoezi ya viungo, Wakipiga vita kiasi, Wakikemea sera ya maji safi na salama, wakinionya kuotea mwanga wajua bila kutambua kwamba wanaenda kinyume na miili yao.
Nina kuhakikishia ukinipa kura yako ya NDIO Mwaka 2025,Mwili wako hautapata hasara kwani matunda na mbogamboga mtakula, hii ni kulinda mwili tu, na kuchochea uzalishaji wa vitamini ya Ulinzi, Vinywaji vya maji safi na salama mtalewa lakini kiasi akiwa pembeni kuhakikisha hakuna anayezidisha kadri ya uwezo wake wakutumia, Miguu tutanyosha, mbio tutakimbia, hewa safi tutavuta, mwanga wa jua tutaota, na Afya bora ndio nimepewa usukani wa Madaraka.
Hakika hakuna bado anayeshawishika na zangu hoja, na hakuna anayekumbuka maumivu aliyopata hospitalini kwa sababu tu ya kuchepusha kura ya NDIO kwangu.
Jamani amkeni kuumwa matumbo na kuharisha sababu kubwa ni kunipinga mimi usafi, Kukataa maji safi na salama.
Kuvimbiwa sio tatizo la kupiga ramli, ni jambo la kunipa kura ya NDIO Mwaka 2025,Na kiasi utapata.
Minyoo sio diri kwa kunipinga chakula bora. Natamani nijipendekeze hata bila kura lakini Taifa halitanitambua,
Ninachoshukuru mmeanza kunielewa shida imebaki, hatanielewaje aliyenilisha bila kiasi, aliyenipa chakula bila kuzingatia afya, aliyeninywesha vinywaji tofautitofauti kwa makubaliano kwamba kura yangu ya NDIO kwake itamwendea.
Mficha maradhi kifo kitamuumbua, Ebu kuwa mwazi na kuacha unafiki chagua upande mmoja ili tutambue wapi utasimama kumtetea mgombea wa upande wako.
Naomba nisimame kwenu Ndugu wananchi, nitambulishe kwenu wagombea mweza wangu japokuwa ni wengi, lakini kuweni wavumilivu kusikiliza hoja zao zenye maana.
WAGOMBEA MWENZA WA MWAKA 2025.
01. UCHUMI NA BIASHARA.
"Nipo mbele yenu kumuunga mkono Rais wangu mtarajiwa AFYA BORA, Ni dhahiri na ni ya kweli anayosema nami nakiri wazi mbele yenu bila msaada wa MHE. AFYA BORA, Kufanikiwa kamwe siwezi.
Maana nitakuwa nimedhoofu, kwa kukosa, chakula bora, mwanga wa jua, kiasi, Mazoezi na hata hewa safi na salama.
Jiadhalini kumchagua aliye kinyume nasi kwa sababu ndiye, anayenizuia nisifanikishe baadhi ya safari zangu kwenda nje, kutafuta wawekezaji kwa sababu amemtambulisha adui kwetu yaani Covid 19.
Lakini nipende kuwa kumbusha, Upendo na wema wa Rais Mtarajiwa MHE AFYA BORA, Utafiti alifanya na akaja kwenu na namna bora ya kujikinga na Covid 19.Alishauri maji tiririka nawa, epuka mikusanyiko isiyo ya lazima na nyingine nyingi,
Naomba kuwasilisha kauli mbiu yetu ni
"UCHUMI NA BIASHARA NI MTOTO WA AFYA BORA"
02: ELIMU
"Hakuna afya bora na hakuna elimu bora, hivyo basi Mwaka 2025,Hakikisha kura ya ndio kwa MHESHIMIWA AFYA BORA.
Nami nina yangu maumivu na mazito aliyenifanyia aliye kinyume na upande wetu, Shule zangu nilifunga, masomo nikasaulika vichwani mwa wanafunzi, Mimba wakatafuta wakijua hakuna tena Elimu
Tuna amini tunaouwezo wakumshinda na kumpinga Aliye kinyume wetu pale tu mtakapo kutukupali na kutupa Madaraka.
Elimu ni Afya, hapana bali Afya ni Elimu, Wengi wanasayansi watakuja kujifunza kwetu kwa namna tu tunavyotunza afya zetu na usalama wa nchi yetu katika suala la Afya na Elimu.
03. ULINZI NA USALAMA
Mali zako, Nchi yako tutalinda kwa mitutu na bunduki lakini tukifika usalama na ulinzi wa afya yako Tunampisha Rais mtarajiwa MHE. AFYA BORA.
Ninayo machache kuwaeleza umuhimu wa kumchagua MHE. AFYA BORA, katika nchi yetu, kupitia kwetu Ulinzi na usalama.
Hospitali zitaja walinzi wa miili yetu yaani chanjo, na madawa ya kila aina, Vifaa tiba sio kilio tena, wa mama wajawazito watakuwa Wameshapata Mkombozi.
Kura yako ya ndio ni kwa MHE. AFYA BORA, Jeuli acha ulinzi ni jukumu lake.
04. KAZI NA AJIRA
Ni vigumu kuchagua mtu ambaye ni mdhaifu katika soko letu la Ajira, maana unaweza usiwe msaada kwa taifa letu.
Tunaitaji vijana wachapakazi na wabunifu na hii inaenda sambamba na uimara wa miili yao.
Hivyo Njia pekee ya kukubalika katika soko la ajira huwezi kumkimbia kumpigia kura MHE. AFYA BORA.
Ni ajabu kuyakubali maumivu yaliyosababishwa na aliye kinyume nasi, kwa sababu alipunguza wafanyakazi makazini, waliojiajiri akawaweka ndani kisingizio ni Covid 19. Ili hali msababishi na yeye Mwenyewe.
05. UHURU WA DINI
Tulitaka kujitoa kumpigia kura MHE. AFYA BORA, lakini tulivyokumbuka kupigwa marufuku kwa ibada makanisani na misikitini, ikatubidii kuwa wapole na wanyenyekevu kama kristo hata kuungana na huyu Rais mtarajiwa.
Kiukweli Maandiko ya dini yana laani sana kitendo cha kuiharibu afya ya miili yetu. Na ni Chukizo mbele yake Aliyetuumba
Kwa Maana alitupa mwaga wa jua bure, pumzi ambayo hatuilipii ushuru, chakula bora cha asili na bei nafuu, maji safi na salama kutoka kwenye chemichemi zetu, na hata siku za Mapumziko akatupa ili tudumishe afya zetu na kutafakari neno lake.
Ni vigumu sana kuabudu ukiwa na afya iliyodhoofu, na hii inatusukuma hata sisi, kuungana kwa maombi kumwombea mtu aliyefikwa na maradhi na huku ndiko kwa muunga mkono Rais mtarajiwa.
HITIMISHO
Madhumuni ya kuleta kwenu maudhui haya ni kuwafahamisheni kitu ambacho ni nyeti sana katika tuwachagua viongozi wetu wakubwa, Afya bora ni kitu na muhimu sana na Ndio kilio cha wananchi wengi.
Mfumo niliotumia kuwasilisha unaweza ukawa mgeni kwenu katika kanuni za uandishi, lakini ni namna ambayo nimeshawishika kuongeza ubunifu, ili uweze kumvutia Ndugu msomaji wa makala haya panga na tamani Kuwa Taswira ambayo ni fumbo kwao.
Mwandaaji :-
©tujuemoja
(David Malunda)
MWANAFUNZI KATIKA CHUO CHA RUCU

Upvote
0