Nahama MMU

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Ndugu zangu wana MMU, nahama hili jukwaa pendwa. Kuwepo MMU kunahitaji akili nyingi, hekima, busara, upendo na kufikiri kwingi. Mwaka sasa umesogea na umri wangu pia.
Sitaki tena kutumia akili nyingi kusuluhisha watu wanaotatizwa na mahusiano yao.
Nahamia Jukwaa la siasa nikapumzike. Kule maswala ya kujadili ni machache tu. CCM, CDM, Mbowe, Slaa, Lowassa na Kikwete.
Naombeni sana tena sana nitumie msemo wa Ustaadhat cacico, NIWACHENI NIPWUMWUZIKE
 
Last edited by a moderator:
Mkuu hutaweza....kama unataka ukose kulala pitisha siku hujaingia MMU
 
Jamani usiende basi hamia jukwaa la picha, huko kwenye siasa ndo kuna stress hadi utachoka na roho yako.
Pole lakini kwa yaliyokusibu huku MMU.
happy new year
 
Karibu sana siasani Bujibuji, wala usifadhaishwe na maneno ya wale waliokosa staha. Mimi ndio kijiwe changu kwa sasa, najaribu kurudia enzi hizo najiunga JF.

Mtu akiandika kwa kuropoka wala usisumbuke naye
 
Mmmm unachezea siasani weye
Muulize Baba V akupe introdakisheni ya siasani ndo ukanyage mguu wako.
 
Last edited by a moderator:
Dah! Bujibuji heri huku. Kule hapafai. Kila siku ni topiki pasua kichwa. Huwezi kupumzika labda uwe unaingia jukwaani tu na kuangalia. Jiandae kutukanwa,kudhihakiwa,kudharailiwa. Kuwa na moyo wa jiwe ndiyo utapafurahia. Ila huwezi kuondoka hivi hivi sababu bado katibu na mwenyekiti hawajaidhinisha baraua yako ya kuhama.
Si unaona mwenzako hamy-d kahamia huku anaanza kulalamika kuhusu tanga.
 
Bujibuji wewe umri wako eti umekwenda unaenda kumalizia siasani.... sawa!
 
Last edited by a moderator:
anataka kugombea ubunge jimbo la rukuvi so anaenda kujiandaa ma mistari ya ushawishi
kam ni lengo yambidi ajiandae ipasavyo... Bujibuji ya kweli haya...?
 
Last edited by a moderator:

Bora uhame ndugu yangu.......mimi nimeshanyanyua virago muda sasa nipo jukwaa la wakubwa.......nimegundua mwaka huu nahitaji kujiimarisha zaidi katika hiyo nyanja......ya utekelezaji......
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…