Nahamia kenya

Nahamia kenya

Sijali

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2010
Posts
2,672
Reaction score
1,814
Baada ya matokeo mazuri ya michezo ya riadha huko Uchina, na Kenya kuibuka ya mwazo na kuzishinda nchi kama Marekani, Urusi Uingereza, nimeona hawa jamaa wanatenda kweli wakati sisi Wabongo ni domo, ujanja-ujanja wa kijinga na wivu wa kike.
Ah, afadhali nihame.Nimechoka kuishi nchi isiyo na ushindani, ghera wala ndoto ya kutangulia na kuwa juu. Hakuna hata uchungu au aibu.
Nakumbukahwa hawa jamaa katika miaka ya sabini tulikuwa twawashinda kaika kila kitu cha michezo...soka, riadha, ngumi, muziki... lakini wamekuja wasanifu eti ni viongozi, wezi eti ni watawala, walevi kuwa wakuu wa idara. Leo hii Tanzania pombe inatangazwa hata kuliko elimu na aspirini.
Haya, endeleeni kunywa mie simo!
 
Back
Top Bottom