Uchaguzi 2020 Naheshimu mchango wa Tundu Lissu ila ni hatari sana watu kama yeye kuwa Rais

Uchaguzi 2020 Naheshimu mchango wa Tundu Lissu ila ni hatari sana watu kama yeye kuwa Rais

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Historia haikuwekwa wazi, kitu ambacho Nyerere alitahadharisha watu wenye misimamo mikali hawafai kuwa viongozi. Hata moja ya sababu ya kumchagua Mwinyi kumrithi ni busara na unyenyekevu wake.

Wanamageuzi hawawezi kunielewa kirahisi ila leo nakuja na mifano rahisi labda sababu wote humu sio wanahistoria.

1. DR Congo ilipofikia ni matokeo ya Waziri Mkuu na mwanaharakati aliyekubalika sana Kongo na wakongo wengi sababu walikuwa mbumbumbu.

Lumumba alitumia nguvu na kejeli, siku ya uhuru alitoa hotuba iliyotoa uhai wake, hakuangalia nguvu za mbeligiji na zake, alijaribu kuzima wakivu waliotaka kujitenga kwa mabavu. Walimsifu kwa hotuba iliyojaa hasira na kisasii lakini haikuwa na uhalisia.

2. Idd Amini Dada aliingia kwa mapinduzi yaliyopokelewa kwa shangwe na Waganda wengi, ila kutokuwa na simile, kumtukana kiongozi wa Afrika Kusini wa baguzi hadharani kwenye mkutano wa OAU Addis Ababa Ethiopia, Kugombana na Israeli na alitumia nguvu kubwa na kupambana na rushwa na uhalifu, hali iliyosababisha kuua hata wasio na hatia na kukosana na wahisani wake kulifanya kuyumba uchumi na kuchukiwa na kila mtu.

3. Tomasi Sankara. Anachukuliwa na mbumbumbu wengi kama mwanamapinduzi mzalendo. Ila wasomi na wataalamu wa uongozi walimchukulia mshenzi na mtu asiyejua lolote. Walituhumu kwa kuruhusu mahakama za watu. Yani jamii tena isiyo na elimu yoyote ya sheria inaweza kutoa hukumu dhidi ya wahalifu. Alizuia kuingia mitumba kwenye taifa masikini ambalo raia hawana uwezo wa kununua nguo. Ndiye aliyesema huwezi kuongoza taifa bila kujifanya kichaa.

Aliuza magari ya serikali akaanza kutembelea baiskeli. Aliuawa kizembe tu na rafiki yake wa karibu. Kweli raisi uzungukie taifa kwa baiskeli?

Wako wengi wanaharakati, akina savimbi, Samora Machel, Adolf Hitler. Hawa ni watu wasiochagua kauli ya kukosoa, wanaotafuta kauli ngumu dhidi ya wapinzani wao.

Watu hao hawapaswi kuwa viongozi wa juu labda watendaji tu ndani ya serikali inayoongozwa na mtu mwenye busara.

Tundu hana la kujifunza kutoka kwa Martin Luther King au Mandela, Walipigania haki kwenye mataifa yaliyoua waziwazi wanaharakati. Kufunga na kuonea watu weusi, ila harakati zao zilikuwa za kupigania usawa na haki na si uongozi, Harakati za Lissu na Chadema nyingi ni za kupigania uongozi. Namnukuu Jemsi Mapalala aliyejikita kupigania wattu.

Mfano lissu alitetea bunge kupitisha sheria ya mafao wakati wabunge wangeweza vizuri tu kulazimisha kikokotoo kuingia kwenye sheria ila hawakufanya hivyo

Tuangalie nukuuu za mandela mwaka 1964 kwenye kesi yake ya uhaini.
Nimekuwa nikipigana dhidi ya utawala unaopendea makaburu, pia nimekuwa nikipinga utawala utakaowapendelea waafrika, nakama hili ni kosa nipo tayari kuuawa.

"Binadamu hazaliwi na chuk bali hufundishwa kuchukia Kama wanaweza kujifunza kuchukia, basi
wanaweza kufundishwa kupenda, kwa
sababu kwa kawaida ni asili yake"
upendo kuja kwa moyo wa mwanadamu
kuliko kinyume chake"

Martini Luther alinukuliwa kwenye nukuu zilizotaka usawa, kama hotuba ya ninandoto. Ndoto ya mwanae kuja kupata fulsa kwa matendo na uwezo wao na si rangi zao.

Pamoja na kupambana dhidi ya tawala katili lakini watu hawa hawakuwahi kutoa nukuu za kuwatolea makali Makaburu au viongozi wa marekani, kusema wazi kuwa lazma waondoke. Ukweli na harakati za kupigania haki zilifanya kuwa maarufu sana na kupendwa na wazungu au ccm kama chadema wanavyowaona.
Tundu hana spich za kuunganisha bali kujenga chuki tu. Hana maono ya uongozi ya kutokuchukia, anaonesha chuki za wazi zidi ya ccm badala ya kuwaita ndugu zetu kutoka ccm ambao kimsigi ni watanzania wenzetu tunaotofautiana mitazamo yeye uwachukulia maadui na huwaita kwa kejeri " maccm"
Kwa maono hayo usitegemee watu hao watukuacha uchukue nchi ili baadae uwaadhibu


Pitia harakati za kiongozi wa upinzani Masood Abiora wa Nigeria mitazamo mikali dhidi ya utwala ulimnyima nchi.
Najua nchi za magaribi haziwezi kukaa nyuma yake
 
Huo uzalendo wa Lisu unatokana na jambo gani?
 
Hayo unayasema mbona hayafanani na lisu mbona km kuna mtu unamlenga
Leo namzungumzia Tundu Lissu. Natamani ajifunze kujenga hoja kama Nelsoni Mandela au Martin Ruther. Zile kauli za maccm, na Lugha kali kwenye nyaraka zake zimenifanya nimuone mwanaharakati zaidi kama mwanamapinduzi John Okelo aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar ila busara za KARUME kujishusha akachukua nchi
 
Huo uzalendo wa Lisu unatokana na jambo gani?
Kusimamia maslahi ya nchi kwa kupambana na sharia mbovu za madini walizopitisha mawakala wa mabeberu akina magufuli kipindi wakiwa kwenye baraza la mawaziri chini ya mwenyekiti wao mkapa.

Lissu uzalendo wake huwezi kuufananisha na hao wafanya maovu waliojificha kwenye koti la uzalendo

Kikwete aliwahi kusema kule Singida kipindi cha kampeni uchaguzi mkuu 2010 kuwa "ni heri Dr Slaa kuwa rais kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge" kwa nukuuu hiyo Lissu ni mwiba mchungu kwa viongozi wahuni wahuni waliojivika umungu mtu

2020 John Walker out
 
Huo uzalendo wa Lisu unatokana na jambo gani?

Wakati anapigania raslimali zetu kama madini, jiwe alikuwa kimya kulinda cheo chake cha uwaziri. Tuonyeshe popote Magu alipohoji ufisadi wa nchi hii kabla hajawa mkulu. Uzalendo haupatikani baada ya kuwa na madaraka makubwa, bali ni nyendo zako zote kwa nafasi yoyote.
 
Siyo unamsema magu kweli?maana hatta yeye alisema kuwa ni "kichaa"na kuwa anapenda kufanya kazi na mawaziri "vichaa"kama yeye!pia kwenye suala la msimamo mkali huwezi kumkwepesha!kupora ardhi ya wanyonge bila kuwalipa fidia na bila kujali wanajisikiaje huku akisisitiza kuwa hata ndugu yake pia alimpora na hakumlipa fidia ni ushahidi tosha kuwa huyu ni 'fundamentalist' yeye ni jiwe! Yeye hashauriwi na ukijaribu kumshauri ndiyo utakuwa umeharibu kabisa!anasema kuwa katiba inamchelewesha kwa hiyo sometime anaamua kuikwepa katiba na kufanya kile anachojisikia kufanya bila kujali sheria wala katiba inasemaje!anasema yeye ndiye mhimili uliojichimbia chini kuliko yote kwa hiyo mihimili mingine yote inapaswa kumsujudia! Hivi mtu mwenye misimamo ya aina hii unamtofautishaje na hitla?na Thomas sankara?na Idd amin?lakini je misimamo yake ina faida kwa nchi? Hilo lijadili mwenyewe na ujijibu mwenyewe! Mi sipo!!
 
Leo namzungumzia Tundu Lissu. Natamani ajifunze kujenga hoja kama Nelsoni Mandela au Martin Ruther. Zile kauli za maccm, na Lugha kali kwenye nyaraka zake zimenifanya nimuone mwanaharakati zaidi kama mwanamapinduzi John Okelo aliyeongoza mapinduzi ya Zanzibar ila busara za KARUME kujishusha akachukua nchi
Ruther ndiye Luther? Kama ndiye basi hukuwahi kumfahamu katu! Kama angekuwa na lugha soft kwa hao mabeberu labda hadi leo ungekuta anaishi! Ila huyo alikuwa extreme kweli kweli!mara mia ya akina Lissu,na ndiyo maana aliwekwa kwenye death row! Na akauliwa kama tu walivyotaka kumuua Lissu! Anza kusoma historia upya na ufanyie marekebisho bandiko lako!
 
Kusimamia maslahi ya nchi kwa kupambana na sharia mbovu za madini walizopitisha mawakala wa mabeberu akina magufuli kipindi wakiwa kwenye baraza la mawaziri chini ya mwenyekiti wao mkapa.

Lissu uzalendo wake huwezi kuufananisha na hao wafanya maovu waliojificha kwenye koti la uzalendo

Kikwete aliwahi kusema kule Singida kipindi cha kampeni uchaguzi mkuu 2010 kuwa "ni heri Dr Slaa kuwa rais kuliko Tundu Lissu kuwa mbunge" kwa nukuuu hiyo Lissu ni mwiba mchungu kwa viongozi wahuni wahuni waliojivika umungu mtu

2020 John Walker out
namchukuliaga poa sana mtu anaejadili "watu"
 
Usidanganye watu lisu kuwa raisi sio hatari,hatari ni WEWE.Unaejitahidi kujipendekeza kwenye serikali ya kidhalimu.inayoua watu,inayoonea watu,inayonyanyasa watu,iliyoshusha uchumi wa nchi,inayoongozwa na dikteta uchwara,iliyo na sera mbovu za uchumi,SASA WEW NDIO HATARI.#bungenidhaifusana#
 
Yaani hakuna muunganiko kati ya kichwa cha habari na kiini cha habari.

Baada ya kichwa cha habari nikawa namtafuta mhusika mkuu katika kiini cha habari, lakini nikaishia kusoma wasifu wa viongozi wengine.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwenyezi Mungu huwa anasimama na watu wake! InshaAllah hii ndoto ije itimie Sikh moja
 
Back
Top Bottom