2v1
JF-Expert Member
- Mar 28, 2024
- 247
- 358
Habari zenu members, mnaweza fikiria chochote kile na mkaandika katika uzi huu.
Nahisi hisia tofauti tofauti kama mwanadamu, nimekaa nafikiria hapa maisha ambayo natamani kuyaishi, napenda sana kuwa na mwanamke mmoja tu maishani mwangu ambaye nitaishi naye na kupata naye watoto na kulea naye.
Kuna muda nafikiria pia kuwa mtu mbaya yani mtu ambaye naweza kutembea na wanawake za watu kama wakijaa kwenye mfumo, sa najiuliza hivi haya maisha yangu Mungu atakuwa ananitazamaje, naamua kuacha kufikiria hivo.
Mwisho wa siku naamua kufikiri kuoa na kukaa na mwanamke mmoja, ingawa ukifikiria hali ya sasa baadhi ya ndoa unaweza usiwe na mpango wa kuoa au kuolewa, ah vyovyote vile.
Kuna muda nafikiria mbona kama utafutaji wangu wa fedha umekuwa mgumu na hata nikipata pesa ni kidogo, nasema wenda ni bahati ya mtu, ingawa wapo wanao nidhurumu pesa zangu, ingawa naumia ndiyo hivo naendelea, nafikiria tena nasema kwanini wasidhurike nikifikiria na Yesu alisema "Yohana 8:7 Nao walipozidi kumhoji, alijiinua, akawaambia, Yeye asiye na dhambi miongoni mwenu na awe wa kwanza wa kumtupia jiwe." Najikuta naacha kufikiria hivo.
Kuna muda napenda kufanya vitu vikubwa na nionekane wa kawaida tu, leo nilikuwa namwangalia mwana fa, anaoneka wa kawaida tu ila ukiambiwa ni bilionea(kama nitakuwa sijakosea) huwezi amini.
Huwa najiuliza hivi vipi siku ya mwisho hiyapa nipo mbele zake mwenyezi Mungu aniambia nilete hesabu ya mambo ambayo nimeyafanya duniani sielewi nitampa nini hata sielewi nafikiria nini sasa.
Kuna muda najihisi mwenye dhambi sana hii huwa inanifanya niwe mnyonge na nimkumbuke Mungu wangu. Naweza kufikiria zaidi ya hapa wenda nikaonekana mwendawazimu ila haya ni kwa uchache.