Nahisi mke wangu anachepukaa! Jamani... ushauriii

Nahisi mke wangu anachepukaa! Jamani... ushauriii

1academ

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2016
Posts
2,316
Reaction score
3,567
Mzuka wana j.f Miaka 2 iliyopita nilianza mahusiano na dada ambaye tunafanya naye kazi sehemu moja, ilikuwa kama utani lakini nilijikuta nampenda. Mke wangu naye ni mfanyakazi, tunaenda kazini pamioja ila nilikua nampitia huyu dada.

Baada ya kuanza naye mahusiano, alianza kumuonyesha mke wangu dharau, anamjibu vibaya, na tukiwa kwenye gari, unakuta analeta stori za ofisini ambazo anajua kabisa kuwa mke wangu hawezi kuchangia. Mwanzoni mke wangu alikuwa analalamika, lakini nilikuwa namwambia ni wivu wake, aache kuwa na wivu "gari ni yangu, huwezi kunipangia."

Kuna kipindi mke wangu aligombana naye baada ya huyu dada kunitumia video za x. akijichezea na mke wangu akaziona. Nilimgombeza mke wangu, kanidhalilisha kugombana na huyo dada, nilikaa upande wa mchepuko. Mke wangu alikaa kimya, lakini tangu siku hiyo ndoa yetu haikuwa na amani tena, niliacha kumpeleka mke wangu kazini.

Nikirudi nyumbani, mke wangu kanuna alikuwa analalamika kila nikirudi lakini kuna nikaanza kuona mabadiliko. Mke wangu alibadilika, ana furaha, haniambii tena mambo ya kumpeleka kazini, yaani kila kitu kimekuwa vizuri.

Nilijikuta napata wasiwasi na nikaanza kumfuatilia. Baadaye nikagundua kuwa kuna gari linakuja kumchukua nyumbani kila siku. Ni gari ya ofisi, lakini kwa cheo chake si wa kuchukuliwa na gari nyumbani. Nilifuatilia na kugundua kuwa dereva alikuwa anampitia mke wangu kabla ya kupitia wafanyakazi wengine.

Nilimpiga marufuku, lakini mke wangu alicheka tu na kuniambia ni gari ya kazini, hivyo hawezi kuacha. Tangu wakati huo sina amani kabisa. Mke wangu hajali, nimegundua tuna miezi 4 hatujakutana kimwili, na yeye halalamiki mazeee, najichua sana siku hizi kwa kutumia mafuta ya vaseline.

Nilimuuliza kwa nini hatutaki kukutana kimwili, akaniambia, "Wewe si una mwanamke wako sasa, mimi namwamini vipi?" Nahisi mke wangu anachepuka, sina ushahidi, ila nahisi tu. Ana furaha wakati namnyanyasa, na kibaya zaidi, hali hii inaathiri mpaka mahusiano yangu mengine. Nimekuwa mtu wa hasira, sijui nifanye nini.
 
Kuna kipindi mke wangu aligombana naye baada ya huyu dada kunitumia video za x. akijichezea na mke wangu akaziona. Nilimgombeza mke wangu, kanidhalilisha kugombana na huyo dada, nilikaa upande wa mchepuko. Mke wangu alikaa kimya, lakini tangu siku hiyo ndoa yetu haikuwa na amani tena, niliacha kumpeleka mke wangu kazini.
Una umri gani mkuu?
 
Hapo ngoma droo
Acha wivu muache afurahishwe huko kwakuwa wewe huwezi kumfurahisha.
Wewe endelea na huyo malaya wako na yeye ana bwana wake.
Ila akili yako ni ya kitoto.
 
Kuna kipindi mke wangu aligombana naye baada ya huyu dada kunitumia video za x. akijichezea na mke wangu akaziona. Nilimgombeza mke wangu, kanidhalilisha kugombana na huyo dada, nilikaa upande wa mchepuko. Mke wangu alikaa kimya, lakini tangu siku hiyo ndoa yetu haikuwa na amani tena, niliacha kumpeleka mke wangu kazini.
Ukomavu wa kifikra!!!🤨🤨

Haupo
 
Kaka ndoa umeharibu mwenyewe...

Ukiamua utaitengeneza upya...

Ukiamua lakini...
 
Nilimuuliza kwa nini hatutaki kukutana kimwili, akaniambia, "Wewe si una mwanamke wako sasa, mimi namwamini vipi?" Nahisi mke wangu anachepuka, sina ushahidi, ila nahisi tu. Ana furaha wakati namnyanyasa, na kibaya zaidi, hali hii inaathiri mpaka mahusiano yangu mengine. Nimekuwa mtu wa hasira, sijui nifanye nini.

Mkuu una ugonjwa wa AKILI, nenda katibiwe haraka sana.

Na stage aliyofikia Mkeo, ni swala la muda tu atakushangaza.

Be a Man, heshimu mke wako. Na kama ulioa ili umnyanyase basi mrudishe kwao.
 
Acha kumwonyesha unaumia, kiufupi kila mtu acheze mechi zake huku ukipangilia mali zako, kwa sababu hiyo ndoa haitorudi kuwa sawa tenaaa
 
Back
Top Bottom