Nahisi muonekano umeniharibia

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Nilikuwa nimetoka shambani kwenye gari nilikaa na binti mmoja mzuri sana alivaa ushungi nikajiambia kwamba nisipoomba namba hapa ntakuwa najilaumu sana hapo baadaye. nikaomba namba nikapewa.

Sasa toka jioni napiga simu haipokelewi usikuwa saa 3 kapokea nilivyojitambulisha tu akakata simu nimetuma sms hajibu nikajua hana vocha nikatuma 3000 bado kimya baada ya kutafakari sana nikasema pengine muonekano wangu ulikuwa wa kirugaruga nilikuwa hivi.

1. Kuna ndugu zangu walinipa squash kubwa sana nilikuwa nimelishika mkononi.

2. Huko shambani nilipewa lita tano za ulanzi nikawa nimebeba kwenye kidumu huu nahisi ndiyo umeniharibia zaidi.

3. Nilikuwa na nokia 105 ye alikuwa na smartphone.

4. Shambani kuna nyoka hivyo nilivaa mabuti kama haya.

Nipeni mbinu wadau, siku zote nilikuwa natafuta kimwana kama huyu siwezi mwacha apite.
 
Hahahaah pole sana. ungetuma kama laki angekutafuta mwenyewe.
 
Ha ha ha ha ha jitetee kwamba alivokuona ulikua umetoka shambani kwako, omba mtoko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…