Nahisi napenda nisipopendeka. Je, ni uamuzi sahihi nilioufanya?

nilikuwa sina raha siku nzima, ila umenifanya nicheke, kamba ishakatika hiyo.
 
Tafuta kiburudisho upotezee mawazo huku ukiendelea kumfuatilia, then akiingia line 'kamua' halafu mpotezee mazima. Ukimfuatilia sana atakuja kujua kuwa unampenda kweli na kama hana mtu atakukubalia, ila na wewe mfanyizie umafya atakapokukubalia. Kwa kuwa amekusumbua muda mrefu, basi akiiingia 'king' kula mzigo halafu mpotezee mazima ili na yeye atie akili kama alivyokusumbua.
 
iyo ilishawahi kunitokea sema nikaamua kumpotezea but after a period alijirudi ila na mm nikamwekea ukauzu, yan mpaka kesho ajaamini kama ni mm... samtyms to give up is strong enough to let samthin go..! ka ukijua sio ww unakosa bahati but ni yeye mwenyew ndo kakosa bahati ya kuwa na ww .. be real
 
mi najua akili mwake, kashajiwekea dhana kwamba nampenda sana na lazima nitamtafuta tu. Kiukwel upendo unazid kupungua kama siyo kwisha kabisa.
 
ni chungu kumeza lakin sina altenative nyingine.
 
Kaka hapo haupendwi. Yaani ukiona unajitahidi kuwasiliana na mwenzio halafu yeye haoneshi ushirikiano ujue umepotea njia.
 
Kaka hapo haupendwi. Yaani ukiona unajitahidi kuwasiliana na mwenzio halafu yeye haoneshi ushirikiano ujue umepotea njia.
ni kweli dada angu, nadhan hili halihitaji hata kusoma "pure adv maths" kuelewa. Ila ni ubish 2 unaoponza akili na mwili.
 
Umeongea mambo ya msingi, hapa nazidi kugundua kwamba mambo mengine ni kujiendekeza, mwanzo nilimfanya oxygen>kumbe nilikuwa najidanganya, hata siamin kama nimemaliza wik 3 pasipo kuwasiliana naye.
Mkuu kuna mara niliwahi kupenda binti lakini yeye alikuwa mguu moja ndani moja nje,sili silali bila kumuona au kuongea nae,nikafanya uamuzi mgumu nikakata mawasiliano,iliuma saana.Masaa,siku,miezi mpaka sasa ni miaka saba.Yeye alidhani utani na alikuwa kisha waeleza shoga zake bila yeye sipumui, alipoona wiki zinazidi akaanza kutuma watu,mara apite home na kuacha barua,mara aende viwanja vyangu(nami nilibadili),simu nilibadili laini kwa kifupi aliteseka sana zaidi ya alivyonitesa.
 

Mapenzi ni "two way traffic" na hapa naona wewe tu ndio unajaribu kwa kila hali kulirutubisha penzi ambalo kwa mwenzako halipo. Hivyo kwa maoni yangu ni bora tu uchukue 50 zako pamoja na kuwa itakuumiza lakini hakuna jinsi nyingine. Pole sana.
 
Kaka tafuta life hawa viumbe ni bahati tu kuwapata. Hata ufanye juhudi gani kama hajakudondokea utapoteza muda na kamwe hatokwambia hana feelings na wewe. Just be a man akupendaye atakuja tu. Usipende kupoteza muda wako kumfikiria kuna siku atakuletea kadi ya harusi na utapoteza mwelekeo wa life kabisaa. Akupendaye hata sekunde moja hakiachi upumue bila kubip japo hata kwa kukosea.
 
nimekusoma mkuu, hakika mnanipa nguvu ya kusimamia kile nilichokiamua
 
Huyo anakupenda ila ana tabia ya woga na ukimya anaona akikutafuta utamwona ni mhuni, mtafute ukikaa naye mweleze majukumu yake na bila shaka atafanya yote utakayomwagiza kuyafanya, inaonyesha huyo bado hajakomaa kama mabinti wa kileo ambao kumwambia mwanaume njoo uninaniii kwao siyo issue.
 
je umewahi kumtamkia dhahiri lengo lako la kumpenda au ni hizo dalili tu? Ebu mtamkie kidhati jibu lake ndilo litakudhirihishia kama anakupenda au la.
 
hayo ndiyo madhara ya kuwa na iddle mind. Keep your brain bussy hata kwa kusoma vitabu. Kwani mwanamke ni yeye tu. Inawezekana na mtu wake anayempenda kwa dhati unataka amsaliti, na ingekuwa wewe ndiyo unasalitiwa??
 
je umewahi kumtamkia dhahiri lengo lako la kumpenda au ni hizo dalili tu? Ebu mtamkie kidhati jibu lake ndilo litakudhirihishia kama anakupenda au la.
nilishamwambia na yeye alikiri kwamba anajua kwamba nampenda, anadai hajapanga kuwa kuwa na mpenz kwa sasa, labda amalize chuo na kupata kazi, ndiyo anaingia mwaka wa kwanza sasa.
 
hayo ndiyo madhara ya kuwa na iddle mind. Keep your brain bussy hata kwa kusoma vitabu. Kwani mwanamke ni yeye tu. Inawezekana na mtu wake anayempenda kwa dhati unataka amsaliti, na ingekuwa wewe ndiyo unasalitiwa??
Bora angekuwa na mtu, anadai hajawai kuwa na wala hana mtu. Kingine sipo iddle kama unavyofikiri, bado nafikir haya mambo hayakwepeki.
 
Huyo anakupenda ila ana tabia ya woga na ukimya anaona akikutafuta utamwona ni mhuni, .
<br />
<br />

hapana mamdenyi, hapo kutafutana sio kwamba wakanjunjane bali kujuliana hali hata kwa msg.
 
ni kweli dada angu, nadhan hili halihitaji hata kusoma &quot;pure adv maths&quot; kuelewa. Ila ni ubish 2 unaoponza akili na mwili.
<br />
<br />
ndio uache ubishi. Mi mwenyewe mtu yoyote kama simpendi simtafuti hadi aanze yeye. Inawezekana wapo wengi kama mimi au inawezekana anaweka pozi ila kwenye kuwasiliana asingechuna namna hiyo.
 
Pole sana. Ila inawezekana kabisa, yeye kwa sasa hivi amefurahi kwamba umepunguzia usumbufu, maana ukipendwa halfu moyo wako haupo hapo, ni kero tupu. Ukiendelea kumfatilia, anaweza kukuonea "huruma", lakini sio kwamba amekupenda. ILA kumbuka kumshirikisha Mungu katika utafutaji wako. All the best.
 
Reactions: BAK
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…