Nahisi nikijichanganya imekula kwangu ushauri wenu wahitajika

scientificall

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2015
Posts
457
Reaction score
328
Leo katika mahakama ya mwanzo nimeshinda kesi ya kusingiziwa wizi, kesi hii ilindhalilisha sana mpaka kufikia hata mimi kukosa amani kutokana na historia nzuri ya maisha yangu kwa wananijua.

Pia kesi imechukua takribani miezi mitatu ina sikilizwa kwani nimeingizwa mahabusu zaidi ya mara 1. Imenifanya mpaka nikapoteza mwelekeo na attention ya masomo yangu hapo chuoni kwani ndo nipo mwaka wa 3 na bado miezi 2 nimalize chuo.

Ilinikosesha umakini katika kuhudhulia vipindi darasani kwani mda wote niliwaza mahakamani kwani mpaka kupelekea kushika kwa corse work za masomo yangu na kutokuhudhulia vipindi kabisa.

Kesi hii ilinitia hofu sana kwani kwa by law za chuo mwanafunzi akishitakiwa anasimamishwa masomo ila kwangu Mungu Mkubwa chuo walisema tusubiri maamuzi ya mahakama.

Pia nimepoteza gharama kubwa sana ikiwemo usafiri na chakula siku zote za kesi.

Leo imesomwa hukumu hivi....

"Mshitaki umeshindwa kuithibitishia mahakama juu ya mashitaka yako kwa mshitakiwa hivyo mshitakiwa huna hatia na kuanzia sasa upo huru"" mwisho wa kunukuu.

Baada ya hapo tulitoka nje maana sikutaka hata kupoteza mda pale.

Je, kwa kuwa sijapewa hati ya mashitaka naeza ifatilia siku nyingine ili nimshitaki na mimi nilipwe fidia au inakuaje? Ushauri wenu jamani mimi sina uzoefu wa kesi.

Na, je kesi ya kudai fidia itasikilizwa hapohapo mahakama ya mwanzo?.
Útaratibu wa kufungua mashitaka upya upoje?

Nawasilisha!
 
Ningekushauri samehe tu kama umetoka salama ni jambo la kumshukuru Mungu zingatia kuyajenga maisha yako haya makesi kwa vijana tunaotafuta sio mazuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…