Nahisi utajiri baada ya Bakhresa kujenga kiwanda cha sukari jirani yangu

MKEHA

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2013
Posts
716
Reaction score
1,143
Juzi kwenye taarifa ya habari ya Azam niliona maandalizi makubwa ya kuanzisha kiwanda cha sukari pale mto Wami.

Nikiwa mkazi wa Matipwili naona kwangu hiyo ni fursa ya kiuchumi mwaka huuKaribuni sana huku kwani hata bei ya ardhi ni ndogo sana.

Karibu ni tuwe majirani na tajiri. Ukikaa karibu na UA waridi huchelewi kunukia waridi. Nadhani ekari zangu 27 ndo utakua mtaji wangu.
 
Hongera kwa kuiona Fursa, itumie ipasavyo.
 
Hii fursa ya mashamba ya kuichangamkia kabla wenye mashamba hawajapandisha bei.

Fursa uliyoiona wewe huenda wengine hawaijui au hawajaiona kabisaaa.
 
Matipwili??? niliwahi kufika huko kwa ndg yangu mmoja mwalimu hapo
 
Subiri pesa Mkuu...mwaka wako huu...
 
Fasta fasta fanya plan usiingie kichwa kichwa. Jua yeye anafanya nini na wwe ufanye nini kama una msumplement usiwe threat
 
Angalia usiishie kuziuza
 
Nimegundua so kila fursa ni fursa. Ndio maana hata wanaoingia madarakani huiona nchi hii ni fursa lakini pindi wanapokalia vitu vyao vya utawala utawasikia wanvyolalama; mara mimi mwenyewe sikutaka nilisokomezewa na maneno mengi kumbe ni baada ya kuprovuuu otherwise
 
Hongera Bakhressa,wewe ndie mwekezaji na mfanyabiashara usie na mawaa,biashara zako zinaonekana,utajiri wako unaelezeka ulivyopatikana,
Kwangu Mimi,wewe ni mfano hai,wa kuweza kuwa tajiri kwa kufanya kazi halali,
 
Mkuu umechimba handaki mapema nini?

Ili uje kuamisha malighafi kiulaini!!
 
Kuna utapeli mkubwa wa ardhi huko balaa, unaweza kutanishwa na afisa mtendaji, na mwenyekiti wa mtaa, wazee wa baraza la kijiji mpaka muuzaji wote FAKE. Siwatishi ila aisifuye mvua....... .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…