Nahitahi partner wa kushirikiana kwenye biashara

plenteous

Member
Joined
Jan 12, 2024
Posts
7
Reaction score
9
Wakuu kama kichwa kinavyoeleza hapo juu muda mrefu nimekuwa na mpango wakufungua car wash pamoja na car body repair ambayo itakuwa na ubora na yenye kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu!

Nashukuru now nimefanikiwa kupata vitendea kazi vyote vinavyohitajika, tatizo kubwa kwa sasa ni kupata mtu wa kuungana nae na kushirikiana naye.

Binafsi naamini katika team work kifupi natafuta mtu ambae majukumu yake makubwa ni kulipia kodi ya eneo ambalo tutalitafuta baada ya hapo tutakaa chini na kuweka makubaliano maalumu ya namna ya kupata faida na tunagawanaje.

Karibu kwa mtu ambae yuko serious tuweze kuzungumza zaidi

Upande wa vifaa niko navyo mpaka sasa kama ifuatavyo.
1. Tank la maji lita 2000
2. Car wash mashine
3. Vacum cleaner
4. Compressor lita 200
5. Headlight cleaner
6. Spray gun
7. Pressure pipe
8. Sanding mashine
9. Livert mashine
10. Pressure gauge
 
Mkuuu! Kama umejitafuta kufikia hapo unashindwaje kumalizia? Partnership business ni ngumu! Inahitaji mtu mliyeshibana! Ndo maana biashara ya jinsi hiyo huusisha ndugu au familia kwasababu wanajimudu wao kwa wao kuliko mtu baki.
 
Mnagawana hisa za kampuni?

Je wewe ni asilimia ngapi za share uko tayari kuzitoa?. Mwekezaji akisema mgawane share 50-50 uko tayari?.

Au unavyosema mtaweka makubaliano maalumu ya kugawama faida una maanisha nini?
 
Uko wapi wewe?
 
Mnagawana hisa za kampuni?

Je wewe ni asilimia ngapi za share uko tayari kuzitoa?. Mwekezaji akisema mgawane share 50-50 uko tayari?.

Au unavyosema mtaweka makubaliano maalumu ya kugawama faida una maanisha nini?
Makubaliano maalumu kwamba kwenye kila faida tutakayo pata baada ya kutoa ghalama za uendeshaji, ndipo tutakaa kukubaliana anachukua asilimia ngapi na chukua asilimia ngapi?!
 
Wakuu Bado mtu ajapatikana yoyote interested plz njoo tuyajenge
 
Wakuu Bado mtu ajapatikana yoyote interested plz njoo tuyajenge
ingekuwa kanda ya ziwa nipo tayari, DSM mbali sana, idea hii hata mi ninayo sijapata msimamizi active
 
Duh. Tokea mwez wa tatu ? Tafuta namna nyingine mkuu.
Partnership na mtu mweusi ni changamoto watu sio waaminifu na pia partnership zinazofanikiwa ni zile wote mshajipata mko vizur mnaungana kuwa nguvu kubwa zaidi hapo changamoto zinakuwa ndogo sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…