Nahitaj mwanamke awe rafiki sana na ikiwezekana awe mke kabisa

Nahitaj mwanamke awe rafiki sana na ikiwezekana awe mke kabisa

Seek

Member
Joined
Oct 26, 2013
Posts
27
Reaction score
6
Awe rafiki sana:
-Niweze kumuamini na kumtegemea pale inapobidi
-Niweze kuzungumza naye hisia zangu bila kificho
-Tushirikiane katika hali mbalimbali inapofaa
-etc..

Ikiwezekana awe mke kabisa:
-Sio lazima awe mke wangu maana kuoa/kuolewa ni mchakato
-Ikishindikana kuwa mke nitalinda na kuheshimu mipaka ya uhusiano wetu
-Ikitokea nikamuoa itakuwa ni ridhaa yetu mimi na yeye. Hata hivyo atakuwa amenifaa kwa kiasi kikubwa maana sio mrahisi ktk maamuzi hayo.


Mimi:
-Nina udhaifu wa kuchelewa kugundua asiyenipenda (asiye nitakia mazuri/mema) maana siku zote natanguliza kumfikiria/kumchukulia mtu kwa uzuri.
-Pia nina udhaifu wa kujitolea kwa rafiki/watu mbalimbali
-Halafu nina udhaifu wa kusema ukweli au kutosema kabisa, lakini sio kudanganya
[Nimeamua kuita udhaifu maana wapo watu ambao kuna wakati maisha huwalazimu kuwa tofauti na hivyo]

-Kwa anaye jali umri;nina miaka zaidi ya 30 na ni pungufu ya 40 (just around 30 yrs)
-Kwa wale wa maumbile; kimo cha wastani (around 5'5"), umbo la kawaida pia (si mnene si mwembamba), rangi nyeusi kiasi.
-Male, never married, and without children
-Na kwa wanaozingatia elimu; nina shahada moja na nitasoma zaidi nitakapo pata wasaa.
-Yes! nafanya kazi, na ninaishi D'salaam

Yeye:
-Nafasi iko wazi kwa kila mwanamke mtu mzima mwenye akili timamu
-Anaweza hata kuwa nje ya nchi (Tanzania), lakini nitaweza kumvumilia kwa muda tu nione kama ni uhusiano wenye mashiko (Nachelea ya wahenga "fimbo ya mbali.......")
-Akiwa mke, ajitahidi kujua kuwaelewa ndugu jamaa na marafiki kama sio kuwapenda au kuwavumilia.... zaidi ni ikitokea wametembeleana
-etc

Karibuni!
...........................
 
Salaam!
Usisahau kutuletea mrejesho hapa hapa!
Salaam!
 
Kuwa na imani utampata umtakae na mwenyewe sifa unazoitaji....
Mtangulize Mungu Kwanza
 
Back
Top Bottom