Nahitaji anayeuza fremu za biashara

Mamujay

Senior Member
Joined
Dec 24, 2022
Posts
149
Reaction score
345
Ndugu zangu nahitaji anayeuza fremu za biashara hata kama nyumba ya nyuma utabaki nayo (Kama ipo) eneo lililochangamka

Aniuzie fremu tu za biashara niwe nazipangisha na kufanyia biashara zangu
 
Hiyo ngumu sana.

Wenzako wanatumia mbinu ya kununua kiwanja kinachofaa kujengwa fremu.

Hata kama ni kidogo wanakinunua tu. Kisha wanajenga fremu na kufanya biashara wanayotaka.

Ni ngumu sana kupata mtu akuuzie fremu zake. Maana fremu zinaingiza kodi kubwa kuliko nyumba za kuishi. Pia fremu zina faida sana kwa mmiliki.

Mbinu ya pili unaingia mkataba na mwenye kiwanja sehemu nzuri zilizochangamka.

Wewe unajenga fremu idadi kazaa.. kisha mnagawana zingine zinakuwa mali yako na zingine mali ya mwenye kiwanja
 
Ndugu zangu nahitaji anayeuza fremu za biashara hata kama nyumba ya nyuma utabaki nayo (Kama ipo) eneo lililochangamka

Aniuzie fremu tu za biashara niwe nazipangisha na kufanyia biashara zangu
njoo hapa big bon kariakoo
 
Kama hujapata na unataka Arusha zipo fremu tano (semi finished) Njiro ndani ya uwanja mkubwa 40m x 48m. Bei 75 mllion
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…