Nahitaji bima ya afya ya haraka

Buntungwa

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2010
Posts
549
Reaction score
307
Wakuu kama kichwa cha habari kinavyojieleza nahitaji kulipia bima ya haraka

Nikiwa na maana kwamba nalipia leo keshoo naanza kuitumia,ni bima gani nzuri

Namgonjwa amelanzwa muhimbili hana bima,anahitaji bima ya haraka ili audumiwe vizuri

Duuu nisaidieni tuu wakuu
 
Mkuu, bima inategemea na uwezo wako, zipo za aina mbalimbali. Jambo la msingi ni kuwa bima ina taratibu zake, mfano NHIF ukishalipia na kupata kadi unaweza kuanza kupata matibabu madogo madogo na vipimo vya magonjwa madogo madogo, ila kama utahitaji kutibiwa magonjwa makubwa mfano matatizo ya figo kushindwa kufanya kazi na kutakiwa kusafishwa damu kwa mashine, hapa ni lazima ulipie pesa hata kama una bima hadi utakapofikisha michango ya angalau mwaka mmoja.

Bima inaendeshwa kwa kuchangiana, wakati wewe una afya njema au umeugua malaria mara moja tu kwa mwaka, ujue pia mchango wako unamsaidia jamaa mwingine mwenye matatizo ya kiafya makubwa yanayotumia gharama kubwa sana, kwa hiyo ni vizuri uwe na bima ya afya mapema ukiwa na afya njema kabla ya kusubiri upate matatizo ndio uanze kufikiria kujiunga na bima.

Nafikiri utakuwa umenisoma Mkuu.
 
Mkuu hive Bima ya NHIF ina ruhusu kupata vipimo vya MRI na CT SCAN
 
Mkuu wewe ni Jipu Bima haitolewi kwa Wagonjwa... Bima ni kwa ajili ya watu wasioumwa ili wakiumwa michango yao itumike... wewe huna tofauti na mwizi... Kamtibie na pesa zako mgonjwa Tambua pia ni kosa kutumia ujanja janja kisha kumkatia mgonjwa Bima akiwa hospitalini... Bima haitolipa gharama hizo
 
watu wengi wanapuuziaga hii kama wewe hapo mwisho wa siku wakipata ugonjwa wanadata
 
Hiyo bima unalipia kiasi gani na kwamda gani mkuu fafanua
 
Yaaan hapo imekula kwenu!Hamna bima ambayo itakubali kulipa gharama!!Yaan ulipie leo kesho aingizwe hasara!!!
Pambaneni tu chief mgonjwa apate nafuuu
 
MOJA YA MASHARTI YA BIMA NI UCHANGIAJIWA MIEZI KADHAA SASA UCHANGIE 50000 LABDA THEN WANAJUA KESHO MRI O CT SCAN THEN U DIE WAPATE HASARA WE ;LIPIA TYU MATIBABU
Asante mkuu kwa ushauri mzuri

Ni ndugu yangu anaumwa amelanzwa muhimbili,hana bima ndio anataka nimkatie ili aanze kuitumia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…