Nahitaji elimu kuhusu funza kama chakula cha kuku

Nahitaji elimu kuhusu funza kama chakula cha kuku

mcharewamwika

Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
10
Reaction score
1
Wadau, naomba msaada wa kupata elimu zaidi juu ya utengenezaji wa funza kama chakula cha kuku. na pia naomba kufahamu kama hawa funza kwa hapa Tanzania wanauzwa, basi naomba kufahamu ni wapi nawweza kuwapata.
 
Kuna Funza na kuna minyoo, funza kuwatengeneza ni rahisi hasa kama una fuga na Ng'ombe pia, cha kufanya chukia kinyesi cha Ng'ombe kirundike mahali halafu mwagia maji kwa wingi halafu funika na karatasi ya anylon na endelea kumwagia maji kwa siki mara mbil, siku ya tatu au nne utakutana na funza wa kutosha chukua lisha kuku. Kuhusu Minyoo mtafute jamaa anaitwa Chasha Poultry Farm anayo
 
Mkuu ukifanikiwa kupata detail zozote abt minyoo tupeane taarifa nw Mimi pia naitafuta kwa ajili ya kuku
 
Pia kuna Mchwa ambao upatikanaji wake ni rahisi sana.
Chimba shimo kulingana na majani utakayotumia
funga mzigo wa majani mfn: Mabua ya mahindi, Majani ya Mnazi
Ukifunga funga na waya pia katikati ya furushi/mzigo wamajani weka kitu kizito kidogo kama chuma. waya utako ufunga atakua na kininginizo kama begi kwaajili ya kutolea shimoni.
Mzigo ukiwa tayari dumbukiza ndani ya shimo mwagia maji alafu funika. Baada ya siku 3 funua na andaa turubali kwaajili ya kukusanyia mchwa, toa kifurushi toka shimoni kung'uta mchwa kwenye turubali ukimaliza rudisha mzigo shimoni na weka maji kidogo. kilasiku unatakiwa kuvuna mchwa kuanzia hapo ukiacha kuvuna unaweza kuta kichuguu.
 
mtafute chasha ni mfugaji mkubwa wa wadudu kwa ajili ya chakula cha mifugo na wadudu
1541662889759.png

1541662910239.png

1541662931324.png

1541662973485.png
 
Back
Top Bottom