Hakuna kinachoshindikana chini ya jua. Inategemea specifications na ubora wa gari lenyewe. Kuna rafiki yangu kauza Raum hivi karibuni 4.5. ila hata ukiangalia kwa macho unaona kabisa gari limechoka hata mngurumo wake.
Nikuambie kitu mkuu? Mtu anaweka price tag ya gari kulingana na sababu mbali mbali. Mfano, Ya mwaka gani, model ipi, ubora wa body na engine, Mileage, na mengineyo. Mtu anayejua gari lake ipo kwenye viwango hawezi kuuza kwa bei ya kutupa, otherwise awe na jambo la haraka sana na ni dharura kama kuokoa uhai au mtu ana kesi imemkaba na anaona jela ilee, so analazimika kuizima kwa namna yoyote hata kuuza gari au shamba kwa bei ya hasara. Na watu wa aina hii ni wachache sana.
Mimi nasubiri mteja taratibu ila kwa uhakika, siyumbi na bei za madalali maana najua ubora wa kifaa changu