Kila lugha ina jinsi ya kujieleza, na si lazima Kila neno la Kiswahili liwe na tafsiri ile ile kwa lugha tofauti.
Mapacha kwa Kiingereza ni twins, Kurwa atatambulika kama the 1st (first) au the older, Doto, the 2nd (second), the younger.
Kwa Kiswahili Sina uhakika tunaitaaje waliozaliwa watatu (triplets), wanne (quadruplets) n.k. Ila wenzetu wana maneno ya kuwatambulisha kwa ujumla wao.
Na katika Kiingereza Kurwa au Doto, si jina rasmi la mtu, ataitwa Ally, Peter Halima n.k., Ila kwa WaTz ni kawaida kuwa ni jina rasmi.