Langu
Member
- Nov 20, 2011
- 37
- 9
Habari za leo wana JF, na wanajamvi wa jukwaa hili kwa ujumla, natumaini nyote mu wazima wa afya na kama kuna mgonjwa na mwenye matatizo mbali mbali basi mwenyezi mungu amsaidie.
Napenda kuwashirikisha hiki kitu na nina matumaini nitapata ushauri mzuri kutoka kwenu na utakao weza kunijenga kwa kile nilichokukusudia kufanya.
Ninaishi Dar es Salaam, nahitaji kuanzisha biashara ya nguo za mitumba, mikoba ya mitumba na viatu (flat shoes) kwa ajili ya akina dada na hata wakina mama tu ambazo zitakuwa na kiwango.
Tatizo langu ni kwamba, siyajui haya masoko ambapo naweza kuwa napata hiyo mizigo kwa jumla ili niweze kuanza na hii plan niliyonayo. Hivyo basi, kwa yeyote mwenye uelewa wa hili anaweza akanisaidia ushauri wa vitu hivi;
i) Ni wapi nitaweza pata soko la mitumba, mikoba na flat shoes, na vipi, hivi vitu vinapatikana kwa sehemu tofauti kwa kila kimoja au sehemu hizo hizo?
ii) Jibu ikiwa ni mkoani, siwezi pata mtu anayeleta kutoka huko na ikishafika huku naweza kuchagua kwa bei nzuri na huwa wanapatikana wapi?
iii) Je kuna watu tu wazuri unaowajua wanaweza wakawa wanatoa hivyo vitu kwa jumla kwa hapa Dar es Salaam ?
Lengo langu ni kwa ajili ya kuingia ndani ya ilo soko na kuangalia jinsi biashara hiyo inavyoenda na kuanzisha hiyo biashara, hivyo basi nitashukuru kwa machache na mazuri uliyonayo/mliyonayo, wanaJF wezangu.
Asanteni na mungu azidi kuwabariki.