Nahitaji kueezeka nyumba ni ushauri gani utanifaa

kuna mahali nimeona 1.8 slope yake sio kali sana
 
Uko vizuri sana ..natamani ningeona huu Uzi kabla ya kuezeka kibanda changu...yaani umepita mle mle...
 
Katika kupima futi hapo kwenye kupima nyumba unahesabu Kwa mizunguko mzima kma najua Kwa upana na urefu maana yake najumlisha futi za urefu na upana?
 
Mkuu nahitaji kupaua nyumba yangu kwa kampuni ya Dragron vipi kwa uzoefu wako ni bati isiyopauka?

Maana mtu wao wa mauzo amenishawishi sana, naogopa kuingia chaka.
 
Mkuu nahitaji kupaua nyumba yangu kwa kampuni ya Dragron vipi kwa uzoefu wako ni bati isiyopauka?

Maana mtu wao wa mauzo amenishawishi sana, naogopa kuingia chaka.
Dah sio kwa ubaya ila Ukishindwa Nabaki, alaf au sunshare achana na hizo takataka nyingine utakuja kulia kilio kisiokosa jina. kuna nyumba imepauliwa na bati za hiyo kampuni hazina hata miaka mitatu bati zimepauka balaa
 
Asante kwa ushauri ngoja niingie sokoni nikacheck mojawapo kati ya hizo mbili (Alaf au Sunshare)
 
Katika kupima futi hapo kwenye kupima nyumba unahesabu Kwa mizunguko mzima kma najua Kwa upana na urefu maana yake najumlisha futi za urefu na upana?
Hapana,
Unatafuta eneo la Kila square ya nyumba yako, afu unajumlisha skwea zote kwa pamoja.

Mfano: Nyumba ya vyumba 3 master, chumba kimoja single,sebule ,dining, vibaraza 2 na public toilet 1

👉Vyumba 3 master vya futi 12×12
Itakua (12×12) × 3 = 288 square Futi

👉Chuma 1 single Cha futi 9×9
Itakua (9×9) × 1= 81 square futi

👉Sebule yenye Futi 15×15
Itakua (15×15) × 1= 225 square Futi

👉Dining yenye Futi 10×8
Itakua (10×8) × 1= 80 square Futi

👉Vibaraza 2 vya futi 5×10
Itakua (5×10) × 2 = 100 square futi

👉Public toilet 1 ya futi 5× 7
Itakua (7× 5) × 1= 35 square Futi

Kisha,
Utajulisha square Futi zote pamoja:-
288+81+225+80+100+35= 809 square Futi

Hizo 809 sqFt ndizo skwea futi za nyumba Yako yote.

Baada ya hapo,
utagawanya hizo square futi Kwa 144

YAANI, 809÷144= 5.62

Kisha utamalizia Kwa kuzidisha Kwa 12.
YAANI, 5.62× 12= 67.42, approximately 68.

Hizo 68 ndizo idadi ya bati zinazohitajika kwenye nyumba Yako yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…