!
!
Salaam wanajamvi hili.
Leo naleta kwa mara ya kwanza shida yangu katika jukwaa hili, hasa kwa wazoefu wa kazi, wajuzi wa sheria za kazi na kwa yoyote mwenye uelewa juu ya "warning letter". Nahitaji kufahamu yafuatayo;
1. Ukishapewa warning letter, na ukawa hukubaliani nayo kwa maana ya kwamba unadhani hukustahili kupewa warning letter, unaweza kukata rufaa? na ikitokea umeshinda rufaa hiyo je inaweza kutolewa katika file lako?
2. Je ukipewa warning letter unatakiwa kuijibu?.....mfano umepokea warning letter leo, halafu baada ya wiki mbili unapokea barua nyingine ya kukuuliza kwa nini hujaijibu warning letter, je hii ni sawa.
Ni hayo tu.
Ahsanteni.