Nahitaji kufahamu Utaratibu wa kuwa Clearing Agent

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Salamu,

Nimgependa kupata ushauri na maelezo wa jinsi ya kuwa a Clearing Agent.

  • Ningependa kujua ni license gani zinahitajika na ni mamlaka zipi zinatoa hizo license
  • Ningependa kujua gharama za process nzima hadi kuwa agent kamili pamoja na gharama zozote za mwaka (kama zipo), mfano license fees.
  • Ningependa kujua kama license hiyo hiyo inakuruhusu kufanya clearing bandarini, posta, airport nk au kila sehemu inahitaji kufanya utaratibu binafsi?
  • Ningependa kujua financial potential ya biashara hii. Kwa wenye uzoefu, fursa zipo wapi?
  • Ningependa kujua changamoto zilizopo unapokuwa a clearing agent na jinsi ya kukabiliana nazo.
  • Na mengine yoyote ya ziada unayoweza kunisaidia.
Natanguliza shukrani.
 
Unataka kufungua Clearing and Forwarding Company au unataka tu kuajiriwa kwenye C&F kama Agent ?
 
Mkuu ipo moja naiuza, kama upo tayari njo inbox tuongee vizuri

Ha! Ebwana hiyo ya kuiuza sidhani. Mpaka kufuatilia rekodi zake, madeni, madai ya kodi, nk. sioni umuhimu wa kufanya hivyo. Labda kama ina wateja, hivi hivi ni bora tu kufungua mpya.
 
Mkuu ni mpya ina miaka miwili tu. Taratibu za kufungua mpya ni ndefu na ngumu.
 
Sawasawa nimekupata. Ngoja nitafakari ila wakati huo huo ningependa unisaidie kwa maswali niliyoyaweka hapo juu.
 
Salamu,

Nimgependa kupata ushauri na maelezo wa jinsi ya kuwa a Clearing Agent.

  • Ningependa kujua ni license gani zinahitajika na ni mamlaka zipi zinatoa hizo license
  • Licence zote za biashara zinahitajika, TRA
  • Ningependa kujua gharama za process nzima hadi kuwa agent kamili pamoja na gharama zozote za mwaka (kama zipo), mfano license fees.
  • Milioni kama saba kukamilisha, na kodi za biashara tu kwa mwaka
  • Ningependa kujua kama license hiyo hiyo inakuruhusu kufanya clearing bandarini, posta, airport nk au kila sehemu inahitaji kufanya utaratibu binafsi?
  • Ndio inakuruhusu, ila lazima upate kibali eneo husika
  • Ningependa kujua financial potential ya biashara hii. Kwa wenye uzoefu, fursa zipo wapi?
  • Mtaji wako na customer care yako ndio kila kitu, na namna ya kutafuta wateja na uaminifu
  • Ningependa kujua changamoto zilizopo unapokuwa a clearing agent na jinsi ya kukabiliana nazo.
  • Mtaji, uaminifu na namna ya kupata wateja, na kuwahudumia kwa wakati
  • Na mengine yoyote ya ziada unayoweza kunisaidia.
Natanguliza shukrani.
 
Asante sana. Ngoja nitafakari halafu nitakucheki.
 
Back
Top Bottom