Nahitaji kufahamu zaidi kuhusu BMW 320i


Uwe makini maana ile sio toyota mfumo wa umeme mwingi ikitoa Alama uitibu kwa wakati service kama yote
 
Mkuu hii mashine naipa heshima nimeitumia miaka ya hapo nyuma ni gari nzuri na zaidi ya comfortable kama mfuko upo vema usiwaze hata mara mbili mbili chukua hiyo mashine angalizo usinunue ya bongo mengi yameshachoka sababu likianza kuumwa mfukoni uwe njema kulitibu. Usinunue from singapore mengi yanakuja na mechanical problems nyingi sanasana ukibagain chukua japan inakuwa rahic kidogo na isiwe imetembea km mingi sana kwenye cc hapo chaguo ni lako Mimi nilivuta from japan ikiwa na kms 63000 mpaka leo bado ni mbichi utafikir npya wazee wanavimbia moshi huko
 
Mkuu, ilikugharimu kitita cha sh ngap kwa ujumla hadi ikatua hapai?
 
Natumia bmw so ntakushaur kutokan na experience

1. Hiyo gari iko chini sana so hakikisha mazingira utakayokuwa unatumia zaid iwe lami tu
2. Hakikisha income yako ni nzur na iko stable kwa sababu spare zetu ni bei kdg unaeza kuta kakitu kadogo then unatajiwa bei ambayo ni hatari na nusu(ingawa tuna faida moja kama ni mtunzaji unaweza jikuta miaka inakatika we unafanya service ndogo ndogo)
3. Ukipata ajali uza gari fasta(especially ukigonga mbele)
4. Hakikisha muda wote gari ina bima kubwa(hili ni muhim sana tena sana ndg siku yakikupata utaelewa maana me bima iliisha nikajiambia tu nextweek nitakata halaf nikapta ajali mbaya kabla sijakata pesa iliyonitoka Mungu tu anajua)


Mengine
1. Gari imara sana aisee kama ni mtunzaji utakaa sana bila kuharibika chochote tofaut na Toyota
2. Ukiinunua piga trip kdg uenjoy raha ya hiyo gari sio kuendesha kwenye folen dar bali tembea kdg masafa
3. Comfotability ndani
4. Hakuna kufanana fanana barabarani sometime mnajikuta wawili tu folen nzima
 
While at it, kuna mtu anajua mafundi wa ECU maarufu kama control box? Kuna control box ya gari moja inasumbua na mmiliki katafuta replacement hadi nje ya nchi bila mafanikio. Nasikia huwa zinaweza kuwa reprogrammed so long as hazipo physically damaged.

Cc. Extrovert
 
Anunue gari ingine tu...Kama mpaka nje ya nchi kashindwa kusaidika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…