Biashara ya nafaka ni nzuri maana ushindani ni mdogo na pia kadri utakavyokuwa unadeliver mzigo mzuri ndivyo unazidi kupanua wigo wa kupata wateja zaidi. Changamoto kuu utakazokutana nazo ni smtms kukosa mzigo make nafaka huwa ni kwa msimu hivyo utalazimika uwe na bulkload store kuepuka kukosa wateja incase watahitaji mzigo nawe kukutwa huna hifadhi. Pia itakulazimu usitulie home bali ni mchakamchaka kwenda mbele kusaka bidhaa! ila kiujumla nafaka inalipa sana na faida yake inaonekana directly tofauti na duka la spareparts. Pia biashara za maduka ni pasua kichwa hasa unapojikuta inapigwa doro kuanzia asbh mpaka jioni na smtms siku tatu no mteja kuja kwa duka!!! lazima uapply kizizi aisee!! halafu ushindani na kuigana kwingi kunachelewesha kupanuka kwa biashara!!
Ni hayo tu mdau nayoweza kukushauri.