Nahitaji kujifunza jinsi ya kumfanya kuku wakienyeji kutaga mayai mengi

Nahitaji kujifunza jinsi ya kumfanya kuku wakienyeji kutaga mayai mengi

BiGDaTa

Member
Joined
Dec 11, 2014
Posts
52
Reaction score
25
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya chakula na wakati mwengine nafanya biashara.

Ni kipindi sasa toka niachane na kuuza kuku na badala yake nauza mayai na nimegundua kama nitakuwa na ujuzi au mbinu ya kuwafanya watage mayai mengi.

Kama wana JF mtanisaidia kujuua ni aina gani ya kuku wa kienyeji ambayo inaweza na kiwango kizuri cha utagaji.
 
Hapo ni ngumu maana kuku kutaga mayai mengi inatokana na aina na chakula ila hawezi kuzaa mayai mengi kuliko kiwango anachoweza tengeneza mwilini mwake
 
Walishe chakula cha layers (chagua kampuni ambayo ni nzuri) hao kuku wako wa kienyeji watataga kilasiku hata kama hana jogoo. Ila ni vizuri zaidi ukawalisha asubuhi hadi saa saba mchana cha kisasa (hapa pia itakusaidia maana watakuwa wameshataga mayai), baada ya hapo waruhusu wakaokote wadudu na nyasi nje hadi jioni warudi wenyewe ndani.
Kila la kheri katika ufugaji wa kuku!
 
ukitoa mayai pasi na kulalia, kuku anatarajiwa kutaga zaidi... kuku mwenye hulka njema ya kulalia hutaga mayai machache japo utayatoa... hatarajiwi kuvuka mayai 200 kwa mwaka hii ni kama chini ya asilimia 60.
kupata zaidi ya hapo unahitaji chotara ..
.
 
Walishe chakula cha layers (chagua kampuni ambayo ni nzuri) hao kuku wako wa kienyeji watataga kilasiku hata kama hana jogoo.

Hivi kwa hapa Tanzania (specifically jijini Dar) ni kampuni zipi zina sifa nzuri ya kutengeneza chakula chenye ubora kwa ajili ya kuku? Kwani naona madukani kuna vyakula vinavyotengenezwa na kampuni mbalimbali lakini tatizo kwa mfugaji linakuwa ni uhakika wa chakula cha kampuni ipi kinakidhi viwango vya ubora wa chakula hicho. Je TBS na taasisi zingine za serikali zinamsaidiaje mfugaji katika kusimamia ubora wa vyakula hivi ili aweze kupata thamani halisi ya fedha yake anayotumia kwa ajili ya kununua vyakula hivi kwa kupata mayai mengi na bora? Naamini kutakuwa na wazalishaji wengine wa vyakula vya kuku ambao wanaweza kuwa wanaweka usanii kwenye uchanganyaji wa chakula na
hivyo kuwaumiza wafugaji.
 
Fuga kuroila, trei moja unauza bei gani? Au unauza yai mojamoja bei gani?
 
Back
Top Bottom