bafetimbi
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 1,085
- 1,741
Wasalaam wazee.
Ni kwa muda mrefu sana nimekuwa nikipenda kujifunza sanaa za mapigano.
Sasa wadau naamini humu kuna wakongwe na wajuzi wa mambo haya mnaweza kunipa ushauri.
Je, ni sanaa ipi ya mapigano iko strong kwa maana ya self defence, sihitaji kuwa mkorofi ila mtu akijichanganya vibaya hilo pigo atakalopewa akasimulie ukoo wao wote.
Nipo Mbeya. Kwa wanaojua mkoa wa mbeya mafunzo hayo nitayapata wapi naomba anijuze.
Kuna ishu iliniitokea juzi siku ya iddi mosi, nikaenda pub moja hivi matata sana kwajili ya kupata ulabu na mbuzu choma kidogo
Sasa nikiwa mule ndani kuna jamaa mmoja tukazinguana vikali tu nikasimama kwajili ya mpambano maana naye alionesha wazi anataka tupigane, nikajipanga mkao wa vita sasa. Eebwanaeeee nilikula pigo moja hivi la ajabu kisha akanimalizia na teke moja hivi nikaona sasa huyu simuwezi maana anaonekana anamafunzo ya kupigana wakati mimi sina. Nikataka kumtwisha chupa la kvant wadau wakaja kuzuia pale.
Na mimi nataka kujua kupigana maana sasa tunakoelekea sio kuzuri.