Nahitaji kujifunza Programming

jangos

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2023
Posts
208
Reaction score
231
Kama title inavosema wakuu

Nataka kuwa developer mnaweza kunsaidia sehemu ya kuanzia
Kama kuna website au group Fulani mnaweza kushare nami.

Mungu awabariki🙏
 
Kama title inavosema wakuu

Nataka kuwa developer mnaweza kunsaidia sehemu ya kuanzia
Kama kuna website au group Fulani mnaweza kushare nami.

Mungu awabariki🙏
Humu humu mkuu. Kuna mengi sana. Kuna wajuzi wengi sana.
Jiunge stack overflw, redet, quora.
You tube ndio chuo kikuu.
Kitu cha kwanza fanya utafiti kwa google search. Uliza kama ulivyouliza hapa kisha soma maoni makala, blog nk.
Kisha utapata muelekeo uanzie wapi.
Usianze tu kusoma nenda you tube pitia tech review. What are the language to start, what are trending languages ?
Baada ya hapo uje sasa kwenye kusoma na njia za kusoma either chuoni au distance au online nk.
Kila njia ina mbinu zake.
Nasisitiza fanya kwanza resear hata mwezi mzima ukipitia makala mbali mbali na wataalamu mbali mbali hasa kama self learner. Hapa utakuwa umejenga msingi.
 
Shukran mkuu umenipa muongozo
 
Hatua 6 za Kubobea lugha flani ya compyuta


Hatua 6 za Kubobea lugha flani ya compyuta
Siko mbali sana kwenye maana hii nimejitahidi kusema nilichokusudia



Computer is any electrical device that take input, process it and give out an output under certain special INSTRUCTIONS and store output for future use.

INSTRUCTIONS kwenye maana ya computer ndio hapo ipo programming, yaani mchakato wa kutengeneza INSTRUCTIONS za kutumiwa na computer.


Kuwa huru kuuliza swali lolote kuhusu programming ili kukuza ufahamu wako kuhusu programming kwa mtu yoyote aliye tayari kukusikiliza.

Mara mtu anapo hitaji kujifunza programming awe mwanafunzi au mtu yoyote swali huwa linakuja atajifunzaje na itawezekanaje yeye kubobea??

Watu hasa wanfunzi huangaika sana na hili kupata jinsi sahihi ya wao kujifunza programming language ( programming language maanayake lugha ya kompyuta) na wengine kuishia kujihangaisha kutamani kujifunza kwa ugumu ndani ya muda mfupi yaani fasta fasta kama wanavyokuwa wanazania wao kitu kinacho sababisha wabaki kuzunguka zunguka katika utangulizi au ujuzi wa awali bila wenyewe kujua.


Wengine wanajaribu kuruka hatua na kujaribu kujifunza hatua za mbele moja kwa moja lakini inakuwa haina msaada wowote na mwisho wa siku ni muhimu kufuata mfululizo wa hatua zinazotakiwa kuweza ujuzi wa programming kwa urahisi.

Kiukweli, Kuelekea kujifunza na kubobea programming language ni rahisi na inachukua hatua kadhaa za msingi lakini tatizo ni kwamba wengi hupuuzia jambo hili kitu kinacho tengeneza ugumu kwa upande wao.

Tuangalie hatua unazotakiwa kufuata ili kujifunza na kubobea programming language.



  • Fanya uchaguzi wa lugha ya kompyuta kulingana na mahitaji yako.
  • Elewa na tengeneza misingi yako kuhusiana na hiyo lugha uliochagua.
  • Hama kutoka ujuzi wa awali kwenda ujuzi wa juu.
  • Fanya mazoezi tena,tena na tena.
  • Tengeneza projects ndogo na kubwa
  • Shiriki code zako na ujuzi wako kwa watu wengine.


Sasa Tuangalie hatua hizi kwa undani zaidi

Fanya uchaguzi wa lugha ya compyuta kulingana na mhitaji yako.

Kitu cha kwanza na chenye kipaumbele unatakiwa kuchagua lugha ya kompyuta kulingana na mahitaji yako kwa sababu kuna mamia ya lugha hizi za kompyuta kama vile Python, C, C++,Java, JavaScript, PHP ,Ruby na nyingine zaidi . Kwa mfano kama ukitaka kujifunza programming ikwa ajili ya kutengeneza tovuti (web development ) unaweza kuchagua lugha kama JavaScript, PHP, n k, kama unataka kujifunza lugha kwa ajili ya teknolojia inayo trendi kama vile AI na ML (Machine Language) unaweza kuchagua Python na nyingine zake.

Elewa na tengeneza misingi yako kuhusiana na hiyo lugha ulio ichagua.

Hapa ni muda wako wa kuelewa mambo yote ya awali ambayo ni muhimu kama vile sifa zake , matumizi yake, syntax zake,data type, variables n.k Hii inaweza kuchukuliwa kama mchakato wa muhimu sana kwa sababu utakutengenezea msingi wa kuelewa undani wa safari nzima ya kujifunza programming, Hata elimu zetu nyingine zinafundisha kuwa kitu cha kwanza ni kufahamu msingi kisha kuendelea mbele mfano kutoka alfabeti hadi kutengeneza aya .

Unaweza kutumia vyanzo vingi vya kujifunza vinavyo pendekezwa kama vitabu, YouTube videos, blogu kwa ajili ya kutengeneza msingi imara


Hama kutoka ujuzi wa awali kwenda ujuzi wa juu.

Huu ni wakati sahihi wa kuchimba zaidi na kuingia hatua inayofuata ya ujuzi wa juu.

Unatakiwa kufahamu kwa undani nadhalia zote ndani ya programming kama vile Pointers, Dynamic Memory Allocation, File Management na Preprocessors kwenye lugha y C au nadhalia ya OOPs , Interface na Packages , Multi threading n.k kwenye JAVA.

Vile vile unatakiwa kupitia kuhusiana na Data Structure mfano Linked List, Stack,Queue, Heap n.k na Algorithms kwenye hatua hii ili kuwa bora zaidi. Kuna platform mbalimbali zipo kwenye mtandao kama vile GeekforGeeks, Javatpoint n.k ambako unaweza kujifunza mada hizi kwa upana zaidi.

Fanya mazoezi tena,tena na tena.

Kama ulivyo msemo” mazoezi huimarisha kufanya kwa usahihi”,,,,,, “Practice makes a man perfect “. Unatakiwa kufanya mazoezi kwa kiwango cha juu kwa kadiri unavyo weza ili kuimarisha ujuzi wako wa lugha ya kompyuta.

Ukiwa mzuri katika hili utapata ujasiri. Kuna namna nyingi za kuimarisha ujuzi huu kama codding challenges.

Tengeneza projects ndogo hadi kubwa.

Wakati tayari umetumia muda wako mwingi katika kufanya mazoezi ni muda sasa wa kusghulika na utengenezaji wa projects halisi.

Kutengeneza project zako mwenyewe ni jambo litakalo kufanya kubobea programming, vilevile unaweza ukachagua kuunda project ndogo na kubwa kwa kadiri unavyo jiskia na unavyo hitaji mwenyewe.

Mbinu bora ya kuunda project ya kuvutia na kibunifu kitu cha kwanza ni kufikiria kwanza tatizo au issue ambayo inaweza kutatulika kidijitali.

Hatua zifuatazo za kutatua tatizo au za kutengeneza project zinaweza kuwa msaada.



  • Tambua tatizo
  • Elewa tatizo
  • Orodhesha suluhisho zinazo wezekana
  • Chambua suluhisho hizo kwa makini
  • Chagua suluhisho ambayo imekuwa bora
  • Tengenezea suluhisho mtindo kwa mpangilio
  • Andaa algorithm
  • Andaa utekelezaji wake
  • Andika programu kuu
  • Kagua programu katika vipengele mbalimbali
  • Kagua na ondoa errors zote
  • Hitimisha.


Shiriki Code na Ujuzi wako kwa watu wengine .

Nimuhimu kushiriki na wengine kama ilivyo ujuzi sikuzote unaongezeka kadiri unavyo shiriki,,,,,, Wakati ukitaka kumfundisha mtu hakikisha umeandaa somo lililopo na atakalo elewa kupitia wewe .

Imeandaliwa na JIKU TECH TIPS

Phone 0682329852

Tukutane katika makala ingine.


Facebook Jiku Jiku

Google Search: Jiku Tech Tips

Jifunze Zaidi Hapa

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…