Nahitaji kujifunza ufundi wa magari

Nahitaji kujifunza ufundi wa magari

Plan Of Action

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
462
Reaction score
382
Wakuu, habari?

Nina imani humu kuna watalaamu mbalimbali wa masuala ya magari.. Nahitaji msaada nijifunze ufundi mbalimbali katika garage yoyote hapa Dar.

Elimu yangu hairuhusu kupitia au kwenda vyuo husika vinavyofundisha.
Naomba mwenye uwezo wa kunipa mafunzo, nifanye kazi walau bila malipo, itapendeza sana.
Msaada wako muhimu sana.

Asanteni sana.
 
Ungesema kwanza una elimu gani au kwanini usiweze kusoma hivyo vyuo vya ufundi?
Mkuu elimu yangu ni diploma ya logistics and transport.

Nalazimika kujifunza haya mambo ili kujiweka vyema katika career yangu maana sina namna.
Msaada wako mkuu,

Niko Dar es salaam, Tabata Mwananchi.
 
shoohenry na wengine wataalamu wa haya mambo naombeni kujitolea katika garage zenu.
Nahitaji sana haya mambo..
Pesa sina wadau... nitajitahidi kufanya kazi kwa weledi...
 
wakuu kwa kweli sijapata msaada wowote mpaka sasa.
tafadhalini, naomba nijitolee kwenu wenye sehemu kama hii ninayo tafuta
 
Back
Top Bottom