Wakuu habari zenu naomba kujua zaidi kuhusu kilimo cha muhogo na changamoto zake na aina bora ya mbegu
Habari
qwairah unapatikana wapi?
Ungependa kulima wapi/shamba lipo wapi?
Muhogo ni zao la biashara na chakula.
Kuna taratibu kadhaa ambazo ni vizuri kuzifuata kwa lengo la kuzalisha kwa wingi.
Mathalani zingatia;
1) uchaguzi wa mbegu bora inayoendana na hali ya hewa ya mahali shamba lilipo.
2) maandalizi bora ya shamba
3) upandaji, upaliliaji na utunzaji wa shamba.
4) Uwekezaji wa mbolea ili kupata mavuno mengi kwenye ekari
5) kudhibiti visumbufu (wadudu na magugu)
6) mazao ambayo unaweza kuchanganya na Muhogo kuongeza uzalishaji katika ardhi (mahindi, maharage, soya, alizeti, Viazi, karanga, njugu...)
7) kuvuna na utunzaji baada ya kuvunwa (post-harvest management)
Karibu
qwairah ujifunze mbinu bora za kilimo na kupata Mbegu Bora za Muhogo. Nitumie namba yako PM.