Baada ya kujikusanya nimeona ni vyema nikawekeza hiki kidogo nilichonacho katika ufugaji wa kuku!
Kama kichwa kivyojieleza, nahitaji kuku wa kienyeji wa malawi kwa ajili ya kufuga. Nimevutiwa na kuku hasa kwa utagaji wa mayai (hii nimesoma kwenye majirida na kutoka kwa watu mbali mbali).
Je, vifaranga watakua wanauzwa bei gani? Vipi malezi yao kwa wenye uzoefu nao?
! Tafadhali nahitahiji msaada wenu katika kulifanikisha hili!
Nakaribisha maoni na michango. Malilachasha poultry na wadau wote karibuni.