Nahitaji kununua gari, naomba ushauri

Machaguo yako yanaonesha kabisa hauna specific options maana hayo magari ni tofauti sana.

Fanya hivi:

1. Unataka gari kwa matumizi gani?
2. Bajeti.
3. Import, yard au kwa mtu?
4. Upo wapi?
5. Una chombo kingine cha usafiri?
6. Kwa siku utakuwa unatumia kilometa ngapi on average?
 
Sema bajeti yako na unataka kwa matumizi gani na pia jaribu pia kufutilia premio na subaru Forester nazo ni gari nzuri
Hizi haziendani kabisa na machaguo yake. Mtu yupo kijijini unadiriki kumtajia Subaru?? Mafundi wa Subaru wapo Mjini pekee, spare mjini na ni ghali; Premio inafaa kwa mtu aliyeko nusu lami na nusu rafu road ila kwa rafu road muda wote sishauri sana
 
Hawa ndio wanaotaka gari kwa kusema nataka namba D au E.
 
Hizi haziendani kabisa na machaguo yake. Mtu yupo kijijini unadiriki kumtajia Subaru?? Mafundi wa Subaru wapo Mjini pekee, spare mjini tu, na ni fupi (ground clearance); Premio haifai kwa rafu road muda wote
Hapana bana, premio nina uzoefu nazo bana halafu subaru Forester ziko vizuri sema sio nzuri sana kwenye rough road na mafundi hawazijulii ila huku Jamiiiforums tusiwe watu wa kupinga tuu bila hoja sasa mawazo yako ni yapi
 
Hapana bana premio ninauzoefu nazo bana halafu subaru Forester ziko vizuri sema sio nzuri sana kwenye rough road na mafundi awazijulii ila huku jamiii forum tusiwe watu wakupinga tuu bila hoja sasa mawazo yako ni yapi
Nasubiri aseme anahitaji gari kwa matumizi gani ili tuweze kumshauri vizuri ILA kwa hayo machaguo yake
  1. Kama anahitaji abebee Vitu au abiria kidogo kidogo achukue Noah japo anatakiwa awe na dereva mzuri na sio kubadilisha dereva kila mara
  2. Na kama ni kwa shuhuli zake tu binafsi achukue Rav 4 tena atafute 4wheels kabisa kwa kuwa yupo rafu road. Hizo toyota RAV4 zinatengenezeka, spare zipo na ni imara
  3. Suzuki ni nzuri na Imara ila bodi yake sio nzuri sana kwa rafu road na spare ni ghali na zanapatikana miji mikubwa tu
 
Aina ya gari ninalotaka iwe noah old au rav 4 old, au suzuki Escudo.

Naomba kujua ipi inafaa kwenye rough road sana. Na ipi ni nzuri kati manual na automatic.
Hamna gari ya rough road kati ya hizo ulizotaja
 
Huku mgololo tunatumia premio ni nzuri kwa barabara zisizo za lami
Hizi haziendani kabisa na machaguo yake. Mtu yupo kijijini unadiriki kumtajia Subaru?? Mafundi wa Subaru wapo Mjini pekee, spare mjini tu, na ni fupi (ground clearance); Premio haifai kwa rafu road muda wote
 
Hivi Rumion zimeishia wapi? Siku hizi sisikii kabisa raia wakizipigia promo humu [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Aina ya gari ninalotaka iwe noah old au rav 4 old, au suzuki Escudo.

Naomba kujua ipi inafaa kwenye rough road sana. Na ipi ni nzuri kati manual na automatic.
Noah SR40 au Toure the best option
 
Mkuu ni kubeba familia tu ndio matumizi makubwa. Na safari za km 80 mara mojamoja
 
Hamna gari ya rough road kati ya hizo ulizotaja
Nipe option mkuu, kama kweli Suzuki Escudo old haiwezi kusurvive kwenye rough road
 
Aina ya gari ninalotaka iwe noah old au rav 4 old, au suzuki Escudo.

Naomba kujua ipi inafaa kwenye rough road sana. Na ipi ni nzuri kati manual na automatic.
Habari yako... Nmeona umepost jamii forum unaomb ushauri juu ya kununua gari... Mm ni agent nafanya Clearing bandarin karibu 0764423726
 
Kila la kheri ngoja waje kukupa muongozo...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…