Tatizo lako jamaa yangu hujasema umesomea nini!! Maana sasa hivi kazi za serikalini ziko nje nje mradi uwe na ujuzi wako uliosomea. Siyo umemaliza "O" level halafu unataka ukafanye kazi serikalini hapo hupati kitu , labda kubeba mafaili kutoka ofisi moja kwenda nyingine.
Lakini kama una cheti chako (Hasa kuanzia Diploma na kuendelea) mfano kilimo, ualimu, mifugo, uuguzi, uganga, Maendeleo ya jamii n.k kazi utapata nenda tu kwenye ofisi ya DED hapo ulipo ukaulizie watakupa ufafanuzi. Maana sasa hivi kila halmashauri inaangalia mapungufu na kujaza hizo nafasi kwa kutangaza. Kwa kweli kwenye NGOs watu wanapataka tu lakini unafanyishwa kazi kama punda tofauti na serikalini kuna fursa nyingi sana mfano kujiendeleza kielimu, kufanya shughuli zako binafsi n.k. kwenye NGOs huo muda utaupata wapi? Hata kufanya kibiashara tu kidogo ni kazi kweli kweli!