Nahitaji kurudishiwa pesa ya installment

Gazaniga

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2015
Posts
1,051
Reaction score
360
Habari wanajamvi

Niliamua kununua mojawapo ya furniture iliyokuwa inauzwa sh.laki8 ila nilimpa muuzaji sh.laki4, na tulikubaliana amalize kuitengeneza kisha nitamalizia pesa. Na risiti ninayo na ina condition kuwa mali ikiuzwa hairudishwi ila mimi bado sijanunua

Sasa,nimehamia mbali na nilimwomba anirudishie pesa na akakubali ila naona sasa ananidhulumu kwani umepita muda sasa ananichenga tu, nataka anilipe pesa yangu kisheria. Je nianzie wapi?

Naomba msaada.
 
Mh! Mimi naona haki yako ni SAMANI, siyo PESA, ongeeni vizuri.
 
Ulivyo mpa hiyo hela aliiweka tu kukusubiria wewe uhamie mbali akurudishie? Wabongo acheni kurudisha nyuma harakati za wenzenu. Wewe tafuta hiyo shilingi laki nne umpe akupe hizo furniture zako
 
Ulivyo mpa hiyo hela aliiweka tu kukusubiria wewe uhamie mbali akurudishie? Wabongo acheni kurudisha nyuma harakati za wenzenu. Wewe tafuta hiyo shilingi laki nne umpe akupe hizo furniture zako

Jaribu kuuliza upate uelewa zaidi wa scenario ilivyokuwa kabla ya kucomment: tulikuwa tunawasiliana naye mara kwa mara na kuna kipindi nilimtuma dogo ampelekee hela iliyobaki ila akakataa kwa madai kuwa ana kazi nyingi.

Mara ameenda kijijini kwao.
 
Jaribu kuuliza upate uelewa zaidi wa scenario ilivyokuwa kabla ya kucomment: tulikuwa tunawasiliana naye mara kwa mara na kuna kipindi nilimtuma dogo ampelekee hela iliyobaki ila akakataa kwa madai kuwa ana kazi nyingi.

Mara ameenda kijijini kwao.

Mkuu hapo kufuatana na maelezo yako bado una mkataba na huyo jamaa. Kisheria party moja ikianza kuperfom contract party nyingine haina haki ya kuvunja mkataba labda kwa makubaliano ya pande zote mbili (Anticipatory breach), na hii pande athirika itakuwa na haki ya kudai fidia. Kutompa huyo jammaa ako installement iliyobaki itakuumiza wewe zaidi, Utakuwa umevunja mkataba. Pia ukimpa hiyo pesa baki utakuwa umeparform party yako katika mkataba wenu, burden itakuwa kwake. Kuhusu risiti iloandikwa pesa hairudishwi inakubana wewe, japo mauzo hayajakamilika (Exemption clause)
 

Nashukuru sana mkuu kwa msaada,ila risiti niliyonayo inasema mali ikushauzwa hairudishwi akimaanisha samani anazouza huyu jamaa
 
Inavyoonesha ni kwamba, huyo muuzaji ashazitumia hela zako na samani ameshaiuza. Ndo zao. Komaa nae tu, ila kukurudishia laki nne zote ni vigumu
 
Nashukuru sana mkuu kwa msaada,ila risiti niliyonayo inasema mali ikushauzwa hairudishwi akimaanisha samani anazouza huyu jamaa

Hapo sikupata vizuri. Kwa scenario hiyo mkuu usiumize kichwa. kawaida mali ikiuzwa maana yake mkataba umekamilika (discharged by perfomance) hatua mliyo nayo ni part perfomance, kwa hiyo ukimpa tu huyo jamaa pesa nay akakupa mali yoko hiyo clause ndo itakuwa bindig. Mkataba ukivunjika kwa sababu ya party moja kutoperfom (breach) hiyo clause haiaply
 
Nashukuru sana mkuu kwa msaada,ila risiti niliyonayo inasema mali ikushauzwa hairudishwi akimaanisha samani anazouza huyu jamaa

Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba, makubaliano yalikua utoe Advance (malipo ya awali) kisha atengeneze hiyo furniture yako na hapo ulitakiwa umalizie pesa iliyobaki.
Kilichofuata ikawa huyo jamaa afanye wajibu wake wa kutengeneza hiyo bidhaa ili umalizie malipo na wewe uchukue mzigo wako, hapo ndipo dana dana zilipoanza, huyo fundi pesa anaitaka lakini hajamaliza kutengeneza bidhaa, hizo chenga zikaendelea hadi ulipohamia mbali na umekata tamaa unaona bora pesa yako irudi (Hapo ni kama nimekuelewa maelezo yako)

Mimi sio mwanasheria ila kimsingi mambo mawili yanatakiwa yatokee hapo, akukabidhi mzigo wako umpe pesa yake iliyobaki au akurudishie ile pesa uliyompa awali. Hiyo risit kuandikwa mali ikiuzwa haina nguvu kwako kwa sababu hajauza mali bado, hakuna kitu alichokupatia wewe.

Nafikiri inabidi ifike mahali tuanze kuwekeana mikataba kwenye mambo yetu mbalimbali, hapo kinackosekana kipengele cha alitakiwa atimize wajibu wake ndani ya muda gani na kama angeshindwa nini kifanyike na kama angetengeneza furniture kisha ukashindwa kulipa nini kifanyike.

Haya matatizo yanatukumba wengi sana na tumeshaumia sana. Ila pakiwa na maandishi mtu hakuoni mbaya, kanuni zinatawala.

Hapo akina Dragoon wachangamkie fursa ya kuelimisha jamii kujua umuhimu wa kuandikishana kwenye mikataba hata kwenye mambo tunayofikiri ni madogo, itaweka nidhamu na kupunguza usumbufu usio wa lazima.
 
Last edited by a moderator:
Samaritan;

Ni kweli kabisa mkuu ndivyo ilivyotokea na kwasasa hata nikimcall hapokei simu kabisa.
 
Last edited by a moderator:
Samaritan;

Umegundua hiyo mkuu eee.

Sasa ndugu yetu atazungushwa sana tu sababu hawakuandikishana mkataba ukieleza mwisho wa makabidhiano ni lini.Inaweza isha hata miaka nane anadai tu.

Na sheria iko wazi, Pindi unapoona kwamba kuna kutoelewana, umeonewa au hujatendewa kihalali katika mkataba unatakiwa ushtaki ndani ya miaka sita tokea siku ambayo hukutendewa sawa, vinginevyo huwzi nenda mahakamani tena baada ya hiyo miaka sita kuomba mahakama ikupe haki kwa sababu ya madhara ulofanyiwa
 
Last edited by a moderator:

Mkuu upo sahihi kabisa, tatizo wengi wetu nikiwemo mimi miongoni hatujui sheria na hatuoni kama ni shida, hapo ndio nnaposisitiza inabidi nyie mliobobea kwenye sheria mchangamkie fursa.

Japo wengi tumeaminishwa kwamba mambo ya kisheria ni gharama, kwa upande wangu naona ni bora nitoe pesa kuandaa mkataba ili kuepusha hasara kubwa au kuepuka usumbufu usio wa lazima.

Mnaweza vile vile kuendelea kuelimisha jamii hata umuhimu wa mambo ya bima za nyumba na vitu vingine vya thamani ila bei zenu ziendane na uhalisia wa maisha yetu ili kuondoa ule mtazamo kwamba mambo ya kisheria ni ya matanjiri tu!
 
Unaweza kuwa na haki ya kudai pesa yako kwa sababu moja ni kwamba mlikubaliana umpe nusu ya malipo na nusu nyingine utaimaliza kazi ikikamilika na iwapo tu mlikubaliana ni lini kazi iwe imekamilika.

Kwa hiyo iwapo muda wa makubaliano umefika naye hakukamilisha kazi basi arudishe pesa au akupe fidia ya kuchelewesha kazi. Unayo haki ya kumdai mpaka gharama za usumbufu.

Msingi wa madai uwe ni kwamba muda tuliokubaliana kazi awe ameikamilisha umepita kiasi mpaka mimi nimeshahama wakati naingia mkataba nilijua kazi ingelikamilika nikiwa sijahamia eneo jingine. Kwa hiyo ikidhihirika kuwa jamaa amekiuka masharti ya mkataba unahaki kudai mpaka na fidia za usumbufu.

Kwa maelezo zaidi twaweza kuwasiliana kupitia pm.

Msaada wangu ni bure....
 
tatizo letu jingine tunaaminiana sana...unaona huyu mshikaji hawezi nifanyia mbaya matokeo yake ndo inakuwa hivi na huna mkataba...
 
tatizo letu jingine tunaaminiana sana...unaona huyu mshikaji hawezi nifanyia mbaya matokeo yake ndo inakuwa hivi na huna mkataba...

Baba enzi za uhai wake aliwahi kuniambia kila kitu kina faida na hasara zake, na hii ni hasara mojawapo ya kuaminiana sana.

Mwisho wa siku kulipa madeni ni KIPAJI, sio kila mtu anacho!
 
Baba enzi za uhai wake aliwahi kuniambia kila kitu kina faida na hasara zake, na hii ni hasara mojawapo ya kuaminiana sana.

Mwisho wa siku kulipa madeni ni KIPAJI, sio kila mtu anacho!

Kweli mkuu kweli ni KIPAJI...kwa kuwaamini watu nimepoteza sana na hadi kupoteza marafiki...natamani kuwa na roho mbaya nisikopeshe tena ila ninashindwa
 
tatizo letu jingine tunaaminiana sana...unaona huyu mshikaji hawezi nifanyia mbaya matokeo yake ndo inakuwa hivi na huna mkataba...

Dada huyu fundi tulikuwa tunamwamini sote nyumbani kwakuwa keshatufanyia kazi nyingi tu,ni vile sasa ana wateja wengi sasa ameanza kutojali na anajua hatupo karibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…