Nahitaji kuwa professional wa Auto diagnostics na Immobilizer system, ni chuo gani naweza somea?

Nahitaji kuwa professional wa Auto diagnostics na Immobilizer system, ni chuo gani naweza somea?

Little Dreamer

Senior Member
Joined
Sep 12, 2017
Posts
180
Reaction score
162
Habari waku, mimi ni kijana nnayejihusisha na ufundi wa magari kwa muda wa miaka miwili na nusu sasa, napatikana Arusha mjini.

Katika shughuli zangu nilifanikiwa kununua Mashine yangu ya diagnosis kutoka China Aina ya Launch X431 V+ na nikaanza kazi ya diagnosis kama extra coz bado nipo nafanya kazi chini ya fundi.

Katika ufanyaji kazi wangu kuna mahala nakutana na changamoto ambazo inakuwa ni ngumu sana kuzitatua na Kuna muda makosa mtu wa kunielekeza kwa usahihi (ukizingatia nipo gereji local ya mtaani), pia nakuwa interested sana na hii fani kiasi kwamba natamani niingie deep zaidi kwenye mambo ya immobilizer, key programming, ECU n.k

Naulizia kama naweza pata chuo ambacho naweza pata ujuzi wa ndani kabisa lakini isiwe nje ya Afrika Mashariki au kama naweza pata mahali au mtu akaninoa kwenye taaluma hii (kama kuna mtu mtaalamu ambaye yupo tayari kunitrain mpaka nikaiva nipo tayari kumlipa ada)

Asanteni, naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom