Nahitaji maelezo kuhusu gari aina ya starlet

parajonse

Member
Joined
Oct 31, 2017
Posts
9
Reaction score
7
Ndugu wanajamvi naomba kuuliza maelezo kuhusu gari aina ya starlet
1.ulaji wa mafuta
2. Uimara wake
3.kustahimili safari ndefu
4.upatikanaji wa spea na gharama

Ahsante naomba msaada wa maelezo tafadhali
 
Hii gari naona watu wengi wanaisifia katika ubora wake wa injini na body, pia ulaji wake wa mafuta upo chini kdg lakini kwenye root ndefu sina maelezo yake mazuri
 
Ninayo namiliki last week end nilitoka nayo kutoka mwanza to geita niliweka 20 ltrs ikiwa empty nikaenda geita nikarudi nikaendelea ni misele mwanza mara PAA km 400 na nilikua full ac na MTU 4 ndani kwakweli vinanusa cc 1330 Jana MTU simjui kanipigia nimuuzie nikamwambia anitafutie kingine kama hiki maana nimefunga nacho ndoa ya kikatoliki
 
Hii gari ninayo mwaka WA 4 SASA .nasafiri nayo kila kukicha Dar Njombe, Njombe Dar na sijawahi kujuta inakula mzigo na mafuta yake naena 1 Lita Km 14 mpaka 15. Inachanganya haraka na ina speed kubwa.
Inavumilia kila Hali. Sijutii kua nayo
 
Hii gari ninayo mwaka WA 4 SASA .nasafiri nayo kila kukicha Dar Njombe, Njombe Dar na sijawahi kujuta inakula mzigo na mafuta yake naena 1 Lita Km 14 mpaka 15. Inachanganya haraka na ina speed kubwa.
Inavumilia kila Hali. Sijutii kua nayo
Mmenishawishi nitafute hiki kidude katanisaidia
 
Nunua mkuu, nimeshakiburuta miaka 4, imara sana kinavumilia mno.
 
Kuna jamaa alitoka nacho musoma kuja njombe, saa moja jion yuko njombe mjin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…