Wasaalam Wana Jamvi,
Kama heading inavosomeka nmeamua kujikita katika kilimo musimu ujao na maeneo yanayonivutia ni hayo niliyoyataja hapo juu
Babati, Mbulu, Njombe na Iringa ni Sehemu ambazo zinapata mvua mwaka mzima na kilimo cha maeneo hayo sio cha msimu mmoja mwaka mzima ni full kulima na Kuvuna
Maombi yangu kwa mtu anaeweza kunipatia/ Kunisaidia kupata mashamba maeneo hayo ya kukodi itapendeza zaidi. Nahitaji hekari 20+
Natanguliza shukurani
Mungu abariki kazi ya mikono yetu
Asantee mkuu kwa Maoni yakoFanya research ya kutosha kabla hujaingia kwa hii industry!! Aliekudanganya kuwa babati, mbulu, njombe na iringa zinapata mvua mwaka mzima eti ni “full kulima na kuvuna” amekudanganya.
Maeneo yote uliyotaja nimefanikiwa kuishi na ninayajua vilivyo! Kusanya taarifa sahihi kabla hujaingia ili usijutie maamuzi yako!
Karibu sana!
Njoo pm..Wasaalam Wana Jamvi,
Kama heading inavosomeka nmeamua kujikita katika kilimo musimu ujao na maeneo yanayonivutia ni hayo niliyoyataja hapo juu
Babati, Mbulu, Njombe na Iringa ni Sehemu ambazo zinapata mvua mwaka mzima na kilimo cha maeneo hayo sio cha msimu mmoja mwaka mzima ni full kulima na Kuvuna
Maombi yangu kwa mtu anaeweza kunipatia/ Kunisaidia kupata mashamba maeneo hayo ya kukodi itapendeza zaidi. Nahitaji hekari 20+
Natanguliza shukurani
Mungu abariki kazi ya mikono yetu
Ni kweli hakuna mvua mwaka mzima ila kuna mabonde mengi yana maji, mfano maeneo ya yakobi, mabindi, kifanya kuna maji teleunaweza kulima msimu wote, viazi vingi hulimwa kiangazi hasa mabonde ya mabindi, awe tu tiyari kwa suluba mana mifumo ya umwagiliaji ni ya kienyeji inasumbua.Njombe naweza nikakusaidia japo nikueleweshe kidogo, Njombe haipati mvua mwaka mzima kipindi cha mvua ni kuanzia October tar 21 za kuandaa mashamba na wale wanaolima vinyunguni yaani tunapanda kwa kumwagilia ndio wanaanza kupanda muda huo..Ila mashambani tunaanza kupanda mwezi November lakini , Mvua zinakuwa nyingi kuanzia November hadi April zinakata...mwezi May mahindi na maharage mabichi tunavuna ila makavu tunavuna June wengine hadi Julai...agost na September tunapumzika hakuna kulima October tunaanza kuandaa mashamba kwa ajili ya kupanda mwezi November...Hivyo ndio ufahamu wangu kuhusiana na Njombe maana nimekulia kule na shambani nimeenda sana