Nahitaji mkopo ili nipate mtaji wa kuanzisha kilimo

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Wadau wapi ntapata kati ya 10m-15m nikalime. Nina kiwanja chenye hati kama collateral pia nina mkataba wa kazi ambao huwa na urinew kila baada ya mwaka.

Mkataba huo una thamani ya 1m kwa mwezi. Nyaraka zote muhimu ninazo. Ninauwezo wa kurudisha laki sita kwa mwezi.

Nimezunguka mabenki wanasema mara hawakopeshi wakulima, mara uwe ni biashara yenye tin number na report inayoonyesha cash flow na mambo kama hayo ambayo nikiwa kama start up ni shida.

Mwenye kuijua bank au taasisi naweza pata huu mkopo anisaidie tafadhali.
 
Nenda ECO bank kuna masharti nafuu ila kwa hiyo M1 na mkataba wako wa 1year huo ndo shida wanaweza wakakupa 5mil also depends hifadhi ya jamii Una bei gani.
 
Nenda ECO bank kuna masharti nafuu ila kwa hiyo M1 na mkataba wako wa 1year huo ndo shida wanaweza wakakupa 5mil also depends hifadhi ya jamii Una bei gani.
Je akiba katika mifuko hifadhi ya jamii inakubalika kama corateral au ikoje? Tufafanulie kiongozi
 
Nenda ECO Mkuu utapata utaratibu mzima but hela ya hifadhi ya jamii inahusika wewe kupata mkopo.
 
umejaribu kuwaona TIB?
sijawacheki TIB. niliwasomasoma wanaanzia 30m na nasikia kuna urasimu sana na hadi business plan yako ipite na upate mkopo unakuta mwaka umekatika. nataka nianze kidogo na niiikisha kuwa fresh ndo ntaanza na watu kama TIB for big money.
 
Malila mnapataga wapi mitaji ya kilimo?
 
Last edited by a moderator:
Malila mnapataga wapi mitaji ya kilimo?

Mimi nilianzia zero kabisa, baada ya kugundua kuwa sikopesheki ilibidi nifanye homework yangu vizuri.
Ilibidi nibadili tabia yangu, ilibidi vyeti vyangu vya shule nifungie kabatini ( niliwahi kuotesha maua nyumbani kwa mtu hapo Bongo, mpaka leo binti wa yule mzee huniita gardener wao, huwa sijisikii vibaya kwa sababu nilikuwa choka mbaya).

Kwa kukudokeza tu, bia ya mwisho nilikunywa 1998 pale Matumbi Bar Tabata, Siku alipokuja Pat Shange Uwanja wa Taifa ndio ulikuwa mziki wangu wa mwisho kushiriki. Elimu yangu ya juu haikunisaidia kusaka mtaji ila ilichangia kidogo. Nilichofanya, ni kwamba ilibidi nirudie utalaam niliopata secondary, yaani shule ya kilimo, na E/K enzi ya primary school.

Nikajitolea sana( miaka kama mitatu hivi,natangaza jina tu,niliwahi kufundisha hadi tuition), na mimi nikashusha vitu ninavyovijua kichwani mpaka vikaonekana. Wakati nafanya yote hayo, vision yangu ilikuwa clear kabisa mbele yangu, yaani picha ya matarajio yangu ilikuwa kubwa na iko wazi.

Sasa, baada ya vitu vyangu kuonekana, nilianza kupata michango ya mawazo toka kwa Watz mbalimbali, wengine nikawa nafanya nao partnership,wengine tunafanya pamoja lakini kila mtu kivyake.

Naomba nikwambie, juu ya yote; niliboresha afya yangu sana,nikaongeza uaminifu kuanzia kwangu mwenyewe na kwa jamii inayonizunguka ambavyo vilipandisha pr yangu. Nikafanya kazi kwa juhudi na maarifa sana mfululizo wa miaka mitano. Walau nikaanza kupata mwanga.

Juu ya yote, Mungu amenisaidia sana.
 
Mimi ningekushauri hivi:

Mosi, kama kilimo unchokiongelea kinaanza msimu wa mwakani usiwaze mkopo. Jipangie malengo ya unatarajia kulima kiasi gani na bajeti kwa makisio itakuwa kiasi gani kisha anza kufanya saving kwa ajili ya kilimo. Kama kweli unaweza lipa laki sita mkopo kwa mwezi, makadirio ya hadi kufikia mwezi wa kumi na mbili ni zaidi ya Tshs 4m. Hii pesa inatosha kwa kuanza kilimo na gharama zitakazoongezeka utazicover na mshahara wako wa mwezi. Kumbuka njia hii inafaa zaidi kwa kilimo kidogo na cha kati (chini ya ekari 30).

Pili, kama unalenga kufanya kilimo kikubwa fanya yote niliyokuambia hapo juu uhakikishe angalau una pesa kiasi ya kuanzia kilimo. Kisha mtafute rafiki, ndugu au jamaa ambaye mnaweza unganisha nguvu na kulima angalau ekari 50 na kuendelea na mlimie pamoja. Mambo muhimu ya kuzingatia kwenye hii njia ni kumpata mtu mwenye commitment ya kweli na malengo yayofanana au kuelekeana. Hii ni nzuri sana mkiifanya kisasa na ikiwa na matokeo chanya utafurahia kilimo lakini pia ikitokea ukapata matokeo hasi shambani basi hautaumia peke yako.

Mwisho, kilimo ni zaidi ya kupata mkopo benki, Kuna mambo mengine muhimu ya kuzingatia na mojawapo ni usimamizi thabiti wa mradi wako wa kilimo. Hii ni changamoto kubwa sana kwa wakulima walioajiriwa, jipange sawia kwenye hili pia sambamba na kupata mtaji wako wa kilimo.
 
ahsante sana kwa ushauri mkuu. nitaufanyia kazi
 
kweli wakulima wanatabu sana. mi mwenyewe najitahidi kusave na nimejiunga kwenye saccos fulani hivi. vipi, siku hizi unakopesheka?
 
Mimi nina mpango wa kulima zao la ufuta mikoa ya kusini hasa mtwara ila nataka kupata mtu ambaye ni mwenyeji wa eneo husika anyeweza kunisaidia kutafuta shamba na pricess zingine
 
Mkuu unaonaje kama tukiunganisha nguvu ili tugenerate mtaji sisi wenyewe?
Mimi mtaji wangu ni;
1) shamba lenye uhakika wa maji
2) waterpump horsepower5.5, 3" na vifaa vyote vya bustani
3) muda na kujitolea kwa moyo wangu wote kuweza kujikita shamba hata kwa zaidi ya miezi 12
4)Uzoefu wa kilimo cha umwagiliaji
5) rafiki ambaye ni afsa ugani aliye tayari kunisaidia kwenye masuala ya kitaalam kuhusu kilimo cha bustani.
Kama upo tayari nakuomba tuanze kilimo cha MATIKITI MAJI ekari 2, tutatumia mbegu ya HYBRID aina ya SUKARI F1 kwa mchanganuo ufuatao;
1)mbegu kwa ekari2 ni sh 520,000/=
2)spacing: shimo 120cm, mstari 150cm na kila shimo miche 2
3) kila shina litazaa matunda 3 tu.
4) gharama za kulima ni sh 150,000/= plus kununua delively pipe 150metres sh 200,000
5) petrol+oil mpaka kuvuna sh 200,000
6)viuatilifu (pestsides) sh 100,000
Kwakuwa hekta1=10,000sqm
Hekta1=acres 2.5
Then kwenye heka 2 ni mashimo 2*4000sqm/1.8sqm=4444
Kila shimo mashina2. Kila shina matunda3
Grand Total ya matunda ni 2*3*4444=26,664.
 
Kwakuwa matikiti ya hybrid ni makubwa kwa umbo, tutaweza kuuza kwa bei ya jumla sh 2000/= kila tunda.
Hivyo kwa awamu ya kwanza tutapata gross profit: 26664*2000=53328000
NET PROFIT:
Cost of production: sh1170,000 + (usafiri chakula na n.k sh 100,000)=1,270,000
Netprofit 53328000-1270000=TZS52,058,000/=
Assume uncertainties incurred during WIP leading to extreme Loss of the expected yield approximately Tsh 20,000,000!
Bado tutarealize faida nzuri ambayo hakika haitatufanya tujutie au kukata tamaa kusonga mbele.
Na ikumbukwe kuwa Water melon huchukua maximum siku 75 tu kutoka kupandwa mpaka mavuno.
Kama unawoga wa kufanya project hiyo, nikopeshe mimi mtaji hapo juu dhamana yangu ni shamba langu ambalo ni ekari 17 ambalo 70% limezungukwa na mto. Ikitokea nimevuna vizuri ntakupa 30% ya ROI na ntakuomba uwe unafanya thoroughly visits kuona maendeleo ya project.
Nikishindwa, awamu ya kwanza na ya pili kama utaniwezesha basi nitalazimika nikuachie shamba.
 
mkuu umechanganua kitaalamu sana nimevutika sana japo naona profit kama ni too good to be true. lakini inaonyesha ni bonge la business. vipi kuhusu mbolea?. shamba lako liko wapi? kwa huko msimu wa kulima matikiti unaisha mwezi gani?.niko interested sana na ngoja nifanye research. pia naomba tutumiane namba za simu.
 
Mkuu shamba langu ni jipya lina rutuba ya kutosha kabisa kiasi cha kutohitaji mbolea nyingine. Ndiyo maana sikuona umhimu wa kujumuisha bajeti yake.
Matikiti ni kilimo cha umwagiliaji make linahtaji maji yaliyodhibitiwa hivyo hulimwa kwa timing hasa kipindi hiki mvua hamna.
Kuhusu hofu ya faida ya kimahesabu, usiogope na ndiyo maana nikashauri tu-deduct Tsh 20M kwenye hiyo faida. Kinachobaki bado ni faida nzuri sana ambayo inatumotivate kuendelea na mladi.
Shamba langu lipo Turiani Mvomero 300kms from DSM.
Kama tutaanza mapema, kunauwezekano wa kulima mara3 kabla ya ujio wa mvua kubwa march 2015.
Usiogope mkuu kila kitu kinawezekana ukiwa na nina na moyo wa kujitoa.
TWENDE SHAMBA MKUU.
 

Mkuu umenihamasisha sana lakini umewahi kifanya hicho kilimo kabla?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…