Nahitaji mkopo wa kuboresha biashara yangu

Kiumbe duni

Senior Member
Joined
Dec 3, 2011
Posts
100
Reaction score
8
Wadau mimi nina biashara yangu grossery ndogo tu ya kawaida, nahitaji mkopo wa m1 nataka kuiboresha zaidi kwa kuongeza viti, meza pamoja na friza moja kubwa. Nisaidieni ni benki gani ninayoweza kupata mkopo kutokana na vigezo nilivyo navyo?. Ila benki ya Accises na nyingine zenye riba kubwa kama hii sizihitaji. Biashara yangu ina leseni.
 
kumbe unawafahamu access bank, basi wewe ni mzoefu mzuri wa mikopo
 
kumbe unawafahamu access bank, basi wewe ni mzoefu mzuri wa mikopo

Sina uzoefu wala sijawahi kukopa benki yoyote ile, ila kuna watu ninaowafahamu ambao wamechukua mkopo ktk hiyo benk ndio wamenipa taarifa hiyo. Hawana longolongo ktk kutoa pesa kama una vigezo huchukui hata siku 3 lkn riba yao ni noma halafu ukiyumba kidogo tu ktk malipo wanakufilisi.
 

Watembelee NMB, wana riba nzuri sana. Kwa kiwango hicho ni takribani laki moja kwa mwaka. Wasiwasi wangu ni collateral utakazotumia! But kizuri ni kwamba hata vitu vya nyumbani na vitendea kazi vya ofisini wanakubali. Kama unavyo usisite kuwaona hao au tembelea MYC4 kwenye www.myc4.com utakutana na wadau huko.

Kila la heri
 
Ahsante sana mkuu, grossery yangu inatosha kama dhamana. Watu wengi wamenishauri niende NMB.
 
ina maana hata mtu ambye sio mfanyakazi wa serikali anaruhusiwa kukopa NMB?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…