Nahitaji mkopo wa Tsh milioni 8

Nahitaji mkopo wa Tsh milioni 8

Habari waungwana wa jamiiforum,

Natumai ni wazima wa Afya na kama kuna ambaye si mzima kiafya basi Allah amfanyie wepesi ili apone haraka inshallh.



Moja kwa moja niende kwenye mada kama ifuatavyo;



Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 30 nina mke na mtoto. Tangu Mwaka 2017 nilipoteza ajira iliyokuwa inanipatia mkate wangu wa kilasiku. Kutokana na elimu yangu kuwa ndogo (form IV) hivyo mpaka sasa naishi maisha ya kuungaunga sijapata ajira sehemu nyingne.

Baba yangu alituachia nyumba na eneo kubwa maeneo ya kigamboni ferry,

Hivyo basi kutokana na mji kukua na ongezeko la wanafunzi kuhitaji hostel nimeona bora nitumie fursa hii iliyopo kwa kujenga vyumba ambavyo nitapangisha wanafunzi wa vyuo kwa kodi ya Tsh laki moja kwa kila chumba.

Plan yangu ni kujenga vyumba vinne vya kuanzia, eneo ni kubwa naweza kujenga vyumba vingi zaidi ila mtaji sina.

Sina kazi wala biashara hivyo kama kuna Taasisi au mtu yoyote aliye tayari kunisaidia naomba anisaidie.

Shida yangu 8 milioni ambayo nimepiga hesabu nimeona inatosha kwa kuanzia vyumba vinne.

Na deni nitalilipa kwa miezi 30 kwa ziada ya Tsh 2 milion

Yaani baada ya miezi 30 (miaka miwili na nusu) nitarudisha 10 Millions

Dhamana za kuweka ipo nyumba nitaweka kama dhamana.

Ahsanteni
Sikukatishi tamaa ila Muombe Mungu humu jf raia watakuchora tu.
 
Back
Top Bottom