Nahitaji msaaada hapa jamani

FYANGUFYOSA

Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
8
Reaction score
2
wana jf habari zenu? natumaini mnafikiri mambo mengi sana juu ya kuwasaidia wa tz wenzetu ili kupunguza ama kuondoa kabisa matatizo yanayowakabili.
mimi nategemea kuwa baba hivi karibuni. mke wangu ni mja mzito wa miezi saba na wiki tatu, anasumbuliwa na tatizo la vidole vya mikononi kupata ganzi na pia miguu inavimba sana. tumeenda hospitali mara nyingi tumeambiwa kuwa hiyo ni hali ya kawaida kwa waja wazito. sasa nahitaji nipate kujua kutoka kwa wana jf (great thinkers) ni nini sababu ya matatizo haya na kwanini inatokea kwa wengine na wanawake wengine haiwatokei.
samahani, nahitaji majibu yenye sababu za kisayansi,
jibu la kwamba ni hali ya kawaida nimeishapewa so ukiniletea hilo utakuwa bado hujanisaidia.
 
nenda google u-search causes of numbness to pregnant women .huwa wanasema ni hali ya kawaida lakini ikizidi sana ni dalili ya kifafa cha mimba au pressure.nitarudi
 
Vipi umeridhika na majibu hayo au bado?
 
bado nahitaji scientific reasons please. hadi naleta hapa janvini nishauliza sana jamani.
 
pole sana ndugu japo wanaita ni kawaida ila siyo kawaida ni tatizo. laweza sababishwa na kuongezeka wa damu mwilini kwa mama,kuongezeka kwa pressure kwenye mishipa ya miguu na mikono kwa ajili ya ukuaji wa mtoto. Mama huweza kuvimba usoni, mikono, miguu nk yaweza pia ikawa ni upungufu wa madini chokaa( calcium),Kusimama kwa kipindi kirefu. kufanya Kazi nyingi katika siku, mlo kukosa potassium ya kutosha, Kunywa kahawa au vyakula na vinywaji vyenye kahawa kwa wingi, mlo kuwa na sodium au chumvi nyingi au ukosefu wa mazoezi hivyo damu kushindwa kusafiri mwilini kwa urahisi. waweza fika TIENS kwa ushauri zaidi au wasiliana nami kwa:-
TEL NO. +255755569494
E-mail: ruhazwentaki@yahoo.com, ruhazwentaki@gmail.com
or visit: http://www.tiens.com, http://www.aftiens.com
TIENS, TOGETHER WE SHARE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…