Sizinga
Platinum Member
- Oct 30, 2007
- 9,374
- 6,857
Ni story ndefu kidogo lakini kwa ufupi ni kwamba bosi wangu wa mradi-Muhindi(Project Manager) kanishutumu mimi kama mwizi iliyopelekea kuninyima allowances zangu na kunipa barua ya onyo(Memo), kitu ambacho nimechukia sana ilhali sikuhusika na hicho kitu na tayari ukweli ameshaujua. Nilimwandikia barua kali ya kuanika uovu na ubabe wake anaonifanyia na anaoufanya ndani ya mradi huo,ambayo niliipeleka ofisi kuu.
Maamuzi ya ofisi kuu baada ya kuitwa huko, yamepelekea mimi kuhamishwa mradi na kwenda kwenye mradi mwingine. Kwenye ile barua niliyompa nilimpa siku 14 awe ameniomba radhi na amenilipa kiasi flani cha fedha, na iwe onyo kwake kukurupuka kuniita mi mwivi. Siku 14 zimeisha juzi na hamna kitu alichokifanya. Sasa naomba msaada wa kumpata wakili kwakuwa hii suala limeniathiri sana mimi na familia yangu, nataka nimburuze huyu ponjoro kwenye vyombo vya sheria ambako haki itaziingatiwa.
Tayari documents zangu zinazothibitisha tukio zima ninazo na zimekamilika. Naomba msaada wa kisheria nianzie wapi au mwenye mtu wa kumfahamu wakili yooyote aniambie nikamuone kwa maelezo ya kina. Kwa sasa nipo hapa daslam.
My Regards.